Wale wa Kibaha Sec School tujikumbushe


Mkuu Ndamwe, umenikumbusha mbali sana na mzee wetu KAKUNI!! mimi nimepitia Kibaha '81 to '83 A level. tulikuwa na marehemu Kazibure, mama schade (RIP) huyu mama alikuwa mjerumani na alikuwa 'anatoka' na wanafunzi, Lwebandiza na gitaa lake... kweli shule ilikuwa murua sana! mzee KAKANI alikuwa mkali kweli kweli na alisimamia shule ipasavyo! duh, it is hard to believe but it is now 26 years since i left kibaha na sijawahi kupita tena kuona shule iko vipi sasa.
 
Wee mkongwe hasa. Chriss Phabby, DJ Kali Kali ... nilikuwa nawasoma kwenye magazeti wakati niko shule ya msingi kijijini. Nadhani wakati naingia mjini walikwishastaafu. Nimesoma comments nyingi za wakongwe humu... Nafurahi mwanakibaha mwenzenu.
Mkuu, unanikumbusha habari ya Mwanalugali, Maili Moja, Picha ya ndege NK.

Bila kusahau weekend tunapanda Zainabu au Scandinavia kuaj SPACE 1900 MBOWE DISCO kwa Chriss Phabby . . . LOL
 
Mzee Hella aliwafundisha chemistry? Alikuwa pia mzuri.
 
I think it was one of best schools .

Wengine tulisoma KiBAHA wakati huo ikiitwa NORDIC TANGANYIKA PROJECT.
Headmaster wetu BERGSON!!!!!! Enzi za Prof. Karim Hirji[ mathematician]; marehemu C. Apson [ DI], Hussein Mtoro, Prof. Bonni Mwaiseje, Wellington Yoram,Grant Mwaipaja ,Brian Sagatwa.etc
 
Heshima yako mkuu
Wengine tulisoma KiBAHA wakati huo ikiitwa NORDIC TANGANYIKA PROJECT.
Headmaster wetu BERGSON!!!!!! Enzi za Prof. Karim Hirji[ mathematician]; marehemu C. Apson [ DI], Hussein Mtoro, Prof. Bonni Mwaiseje, Grant Mwaipaja ,Brian Sagatwa.etc

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hizo uduma kwa sasa hata private school huzipati
 
ni KAKUNI = KAZI + KUSOMA + NIDHAMU
 
WENGI NI WATU WAZITO SANA nchi hii, nawakumbuka kina Arthur Lyatuu, kina Pius Macha, ....kina Jacob Mtui alikimbizana sana na kile kichwa cha kihindi Salim Ghulam japo Salim alikuwa anawasha taa mbaya sana

ile batch ya kina Kamgisha Kazaura ilichangamsha sana kambi na hasa kule kwenye basket ball. ilikuwa very social na ilizingatia umwamba wa darasani..yaani kupasua ilikuwa fashion

Walimaliza pepa yao ya mwisho wakasherekea sana na kale karedio chao lilkuwa pale skandia ilikuwa ya yule marehemu msukuma flan mweusi kinational panasonic kina spika mbili..walicheza ule wimbo "I ve thinking about you" ..tuliobaki o level tulisikitika sana miezi mitatu na sisi tuondoke..

by the way kuna timu ilikuwa kali sana ya soka form four ya 92 wana "WASA"....... ilitisha sana kina alfred peter chiwachi hatareeeee. boli ilikuwa inapigwa sana pale uwanya wa shirika. kukiwa na ligi tunahamia uwanja namba 2 mpaka 3 baada ya uwanja wa basket kama unaenda mwanalugali

table tenis Benard Taabu Michael

kulikuwa na kaka wawili wakubwa walicheza sana mpira pale timu ya shirika. yule mmoja aliitwa Swai sijui alienda wapi?
mnakumbuka kisa cha Safina na yule James?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…