Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dah!
Mimi hapa mwenzioAse mi nimgumu sana kupiga simu inaweza pita hata mwezi nisipige simu nyumbani au kwa wakwe,jukumu hilo analifanya wife haiwezi pita siku mbili hajapiga simu kwa ndugu zangu na zake wote
Wamesema nahisi wamechoka,
Kuna watu kweli wenye tabia kama zangu
Tuko wengiMwenyewe na kauvivu flani kupiga cm hata sms kumtafuta huwa nasemaga ngoja nitamtafuta Kesho au baadae hapo ndio imetoka...Lkn ikitokea mtu kanipigia au katum sms nakuaga na story nyingi yaani Hadi anasahau kama simtafuteg
Introverts V/s extroverts..Ase mi nimgumu sana kupiga simu inaweza pita hata mwezi nisipige simu nyumbani au kwa wakwe,jukumu hilo analifanya wife haiwezi pita siku mbili hajapiga simu kwa ndugu zangu na zake wote
Wamesema nahisi wamechoka,
Kuna watu kweli wenye tabia kama zangu
Atleast you 2 months...Mimi naweza kaa miaka sijaongea na mzee mpaka najihesabiaga sina baba.Mimi hili suala linanitatiza kwa sasa....sina mazoea na mshua....hajanilea kwa kunijengea urafiki na yeye. Mpaka nimefika utu uzima mimi na mshua hatunaga stori kabisa.
Naweza kukaa 2 months sijampigia simu..na yeye hajanipigia pia na nikawa comfortable kabisa.
Uko kama mimiAse mi nimgumu sana kupiga simu inaweza pita hata mwezi nisipige simu nyumbani au kwa wakwe,jukumu hilo analifanya wife haiwezi pita siku mbili hajapiga simu kwa ndugu zangu na zake wote
Wamesema nahisi wamechoka,
Kuna watu kweli wenye tabia kama zangu
Dah nina huu ugonjwa aiseeMtu unaona kabisa simu inaitaj ila hupokei
Na hauna sababu
Tumepata mbinu apaa ambayo nimeanza kutumia
Waathirika wa kupiga Puli ndio mnawaitaga INTROVERTS kwa kitaalam?Kwenye haiba za watu kuna makundi mawili. Kuna introverts n extroverts.
INTROVERTS hawa ni watu ambao ki asili maisha yao yako ndani, ni watu wa kuishi ndani tu na sio wepesi kuelezea hisia zao. Anaweza kuwa na jambo zuri kabisa la kushauri ili mfanikiwe lakini hasemi, hupenda kutumia muda mwingi peke ake akifany yanayomuhusu tu na ana amani. Huyu hutamuona mtandaoni sijui fb au insta kifupi maisha yake ni full of paswod.
EXTROVERTS Hawa ni watu ambao maisha yao ni gazeti, akiumwa mafua ntaa mzima watajua, akifurahi au kuchukua wote watajua. Misha yake hayana fence. Ni waongeaji sana sana yani ukipanda nae kwenye daladala Kibaha hadi kkoo tayari atakua kakusimulia kila kitu, alisoma wapi, mkewe yukoje n kila faili atasimulia.
MWISHO Ni vyema kujifunza ku balance haiba zetu. Mtu wa asili y ndani ajifunze kutoka na nje pia mana ana mwili. Na yule mwenye asili y nje basi sisahau pswd maan kuna mambo akiyasema yataharibu
Mke wangu ndio kazi yake hiyo,kila siku anawasiliana nao,kuna siku kaniambia Nyumbani wanalalamika wanakupigia simu hupokei nikamwambia nilikuwa mbali na simu baadae muda ukawa umeenda nikaona nisiwasumbue. Ila kashajua huu ni ugonjwa wangu so sometimes anamalizana nao yeye mwenyewe.Tumepata mbinu apaa ambayo nimeanza kutumia
Uwa nahakikisha simu ya wife ina Salio bundle na dakika
Sasa kazi ya kuwajulia Hali ni yake [emoji28]
Na wanawake wanapenda
Apa jioni napewa tu report
Leo bamkubwa anaumwa
Mama janeth anabatiza mtoto kesho
N.k at least nna taarifa [emoji28][emoji28]
Wewe utakuwa na matatizo aisee, hii ni too much mzee [emoji3]Mimi sio kupiga tu hata kupokea sipokei simu za watu na hata sijui ni kwanini, ndugu wote walishanisusa kunipigia simu, hata mtu akiwa na shida anampigia wife aniambie, hata sijui tatizo ni nini?
Kiubinaadam si sawa chief, mcheki jamaa..Tupo wengi Mkuu. Kila Mamamkwe anaponipigia simu lazima nitumie dakika tatu mpaka tano naomba msamaha kwa kutompigia simu na kuahidi kujirekebisha. Lakini bado niko vilevile. Wiki ya tatu sasa, rafiki yangu wa damu wa utotoni kapata ajali ya gari na kulazwa hospitali huko Dar. Sijawahi hata kumpigia simu wakati vocha ninayo. Nasoma tu tarifa zake kwenye group letu la WhatsApp!
We mzee kama mimi. Hivi sijui shida ni nini. Mana mimi huwa sipokei simu, shida wanapiga kwa wife afu wife nae ananipa tu ongeaa....hahahahaha mungu atusameheeAse mi nimgumu sana kupiga simu inaweza pita hata mwezi nisipige simu nyumbani au kwa wakwe, jukumu hilo analifanya wife haiwezi pita siku mbili hajapiga simu kwa ndugu zangu na zake wote.
Wamesema nahisi wamechoka,
Kuna watu kweli wenye tabia kama zangu