Habari Wakuu,
Nianze moja kwa moja kuzungumzia kuhusiana na mada tajwa, mimi ni mkulima na pia nafanya biashara ya kununua mahindi kisha naweka store kwa muda nikisubiri bei iongezeke...
Miaka michache iliyopita hadi kufikia mwaka jana 2017 kipindi kama hiki cha mwezi januari, bei huwa tayari imepanda ambapo utakuta gunia moja la kilo 100 linauzwaTsh. 70,000 hadi 100,000 kulingana na eneo husika.
Mwaka huu hali ni tofauti kabisaa, hali ni mbaya mbaya sana yani hadi sasa gunia la kilo 100 linauzwa Shilingi 40,000 pesa ambayo ni sawa na bei ya kununua mwezi july na august ambapo ni msimu wa mavuno. Ila ikumbukwe hapo tayari kuna gharama za storage, madawa, ulinzi nk.
Mbaya zaidi kuna baadhi ya mikoa kama Mbeya na Mara wakulima wanatarajia kuanza kuvuna mahindi siku za karibuni.
Tujadaliane la kufanya ili kujikomboa kwenye hizi changamoto...hivi unawezaje kuingia shambani wakati mazao uliyonayo bado hujayauza na hata ukiuza pesa utakayopata haitoshi gharama za kilimo?
Swali la msingi ni Je tunafanyaje???
Kutokana na hali ilivyo sasa ni mazao gani ambayo iwe kwa kulima ama kununua na kuweka store kwa muda yana uhakika wa kukupatia faida baadae?????
Suala la kuniambia niyaongezee thamani kwa maana ya kusaga unga, mtaji wangu ni mdogo wa kununua mashine ya kusaga na kufanya packaging ya unga...
Tujadiliane.