Wale Wakulima/Wafanyabiashara tuliopata hasara kutokana na biashara ya Mahindi tukutane hapa

mongoya

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2014
Posts
298
Reaction score
120
Habari Wakuu,

Nianze moja kwa moja kuzungumzia kuhusiana na mada tajwa, mimi ni mkulima na pia nafanya biashara ya kununua mahindi kisha naweka store kwa muda nikisubiri bei iongezeke...

Miaka michache iliyopita hadi kufikia mwaka jana 2017 kipindi kama hiki cha mwezi januari, bei huwa tayari imepanda ambapo utakuta gunia moja la kilo 100 linauzwaTsh. 70,000 hadi 100,000 kulingana na eneo husika.

Mwaka huu hali ni tofauti kabisaa, hali ni mbaya mbaya sana yani hadi sasa gunia la kilo 100 linauzwa Shilingi 40,000 pesa ambayo ni sawa na bei ya kununua mwezi july na august ambapo ni msimu wa mavuno. Ila ikumbukwe hapo tayari kuna gharama za storage, madawa, ulinzi nk.

Mbaya zaidi kuna baadhi ya mikoa kama Mbeya na Mara wakulima wanatarajia kuanza kuvuna mahindi siku za karibuni.

Tujadaliane la kufanya ili kujikomboa kwenye hizi changamoto...hivi unawezaje kuingia shambani wakati mazao uliyonayo bado hujayauza na hata ukiuza pesa utakayopata haitoshi gharama za kilimo?

Swali la msingi ni Je tunafanyaje???

Kutokana na hali ilivyo sasa ni mazao gani ambayo iwe kwa kulima ama kununua na kuweka store kwa muda yana uhakika wa kukupatia faida baadae?????

Suala la kuniambia niyaongezee thamani kwa maana ya kusaga unga, mtaji wangu ni mdogo wa kununua mashine ya kusaga na kufanya packaging ya unga...

Tujadiliane.
 
Ni wakati umefika wa kuongeza thamani ya mazao kwa kuanza biashara ya kukoboa na kusaga mahindi ili uuze unga na pumba
 
Hata bei ya unga iko chini,
kwahiyo labda wabuni mbinu ya kutengeza mikate ya unga wa sembe,keki,maandazi etc.
Kinachotakiwa ni innovation tu kugundua kiungo cha kuufanya mkate wa sembe uwe mkate kweli kweli
 
Akisaga na kuuza sembe atapata faida tofauti na akiyauza Kwa hasara japo faida haitokuwa Kubwa sana lakini hatokula wali mkavu na atakuwa ameongeza maarifa mengine ya ujasiriamali.
 
Huku kwetu debe wanauza 6500 na Wateja hamna coz mwezi wa pili tunavuna na mahindi yamekubali sio mchezo
 
Habari Wakuu,

Nianze moja kwa moja kuzungumzia kuhusiana na mada tajwa, mimi ni mkulima na pia nafanya biashara ya kununua mahindi kisha naweka store kwa muda nikisubiri bei iongezeke...

Miaka michache iliyopita hadi kufikia mwaka jana 2017 kipindi kama hiki cha mwezi januari, bei huwa tayari imepanda ambapo utakuta gunia moja la kilo 100 linauzwaTsh. 70,000 hadi 100,000 kulingana na eneo husika.

Mwaka huu hali ni tofauti kabisaa, hali ni mbaya mbaya sana yani hadi sasa gunia la kilo 100 linauzwa Shilingi 40,000 pesa ambayo ni sawa na bei ya kununua mwezi july na august ambapo ni msimu wa mavuno. Ila ikumbukwe hapo tayari kuna gharama za storage, madawa, ulinzi nk.

Mbaya zaidi kuna baadhi ya mikoa kama Mbeya na Mara wakulima wanatarajia kuanza kuvuna mahindi siku za karibuni.

Tujadaliane la kufanya ili kujikomboa kwenye hizi changamoto...hivi unawezaje kuingia shambani wakati mazao uliyonayo bado hujayauza na hata ukiuza pesa utakayopata haitoshi gharama za kilimo?

Swali la msingi ni Je tunafanyaje???

Kutokana na hali ilivyo sasa ni mazao gani ambayo iwe kwa kulima ama kununua na kuweka store kwa muda yana uhakika wa kukupatia faida baadae?????

Suala la kuniambia niyaongezee thamani kwa maana ya kusaga unga, mtaji wangu ni mdogo wa kununua mashine ya kusaga na kufanya packaging ya unga...

Tujadiliane.
Yauze yote kabla haijashuka zaidi,huwezi kwepa hasara kwenye biashara, matikiti na nyanya ziliunguza hela,lkn msimu uliofata zilitapisha hela ndefu.ujapata hasara we si mfanyabiashara,uza tunza hela jipange upya,mwaka huu chakula kingi sana mvua zinanyesha vya kutosha.
 
Hata bei ya unga iko chini,
kwahiyo labda wabuni mbinu ya kutengeza mikate ya unga wa sembe,keki,maandazi etc.
Kinachotakiwa ni innovation tu kugundua kiungo cha kuufanya mkate wa sembe uwe mkate kweli kweli
IPO teknologia ya kukamua mafuta ya mahind.mafuta bado bei iko vizuri
 
Mwaka huu tumebananishwa. Tusaidiane kutafuta soko la mashariki ya kati kwa ajili ya chakula cha ndege na wanyama
 
Natafakari kwa kina sana!hivi hasara hii imesababishwa na nani!!!???
Ni nature ya biashara au kuna sehemu tulikosea!!!??
 
Hata bei ya unga iko chini,
kwahiyo labda wabuni mbinu ya kutengeza mikate ya unga wa sembe,keki,maandazi etc.
Kinachotakiwa ni innovation tu kugundua kiungo cha kuufanya mkate wa sembe uwe mkate kweli kweli

Hahahaha nisamehe mkuu nimejikuta nacheka tu
 
morogoro naskia gunia ni 53000/= mwaka jana lilifika laki 1 !hatari tupu !na mwaka huu dalili ya chakula kuwa kingi ipo kwa mvua hizi !
 
Inatia hasira sanaaa!!!
Wengi walitegemea bei ingepanda kipindi kile Kenya inayahitaji bei ilikuwa juu shida ikawa mipaka imefungwa mshindi hayatoki,waliporuhusu kutoka nje,wakakuta Kenya ana mahindi ya kutosha baada ya kuagiza kwingine,wakati huo Kenya ni msimu wa mavuno.Pia huku kwetu mvua zinanyesha kuna maeneo wanavuna mahindi. Hivo kupelekea kufurika kwa mahindi. Ni hasara kwa mfanyabiashara faida kwa walaji unga bei chini.
 
Akisaga na kuuza sembe atapata faida tofauti na akiyauza Kwa hasara japo faida haitokuwa Kubwa sana lakini hatokula wali mkavu na atakuwa ameongeza maarifa mengine ya ujasiriamali.
Unamuuzia nani hiyo sembe !??
 
Back
Top Bottom