Wale waliowahi kuchangia room Guest na mtu usiemuelewa ambaye ni jinsia tofauti wakati wa kuwa safarini...

Alikuwa mwembamba sana
 
Kutembea na condom kwenye wallet sio dhambi, dhambi mke/GF kuiona bana!..
Kuna baadhi ya wawakilishi wetu wanatuangusha, heri ya Castr anawakunja hata vyoo vya dreamliner!.
Mkuu hii post yako nimecheka mwenyewe usiku huu watu wamelala[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Tulipotoka ni mbali sna kulipo palipobakia ndo maana tukaamua wote tu rest kwa vile tuliulizia tukaambiwa safar za huko usafair had saa moja usiku unapatikana hakukua na sabbu ya ku rush while exactly reporting day ya target area ni monday
Acha hizo, labda huyo demu hakukushawishi tu ukaamua kumpotezea.Ungekutana na mtoto wa ukweli usingechomoka mkuu
 
Unafua nguo zako za ndani ?
 
Naona PaKa Ulilinda Shombo.



Maumivu yake najua bado unayo,,umekuja kijifariji tu labda huyo dada sura ya baba,,,

Ninauhakika huyo dada alikuwa mzuri ndo maana ukataka kushare chumba!!!
 
Kuwaza ngono tu ni kuharibikiwa akili.

Niliwahi kusafiri kwenye basi kwenda Arusha, tulipandia njiani na dada mmoja na basi likafika usiku saa 4 hivi. Huyo dada alikuwa anaenda Karatu na hajawahi kufika hata Arusha na akadai hana hata hela ya guest na nauli ya Karatu ilikuwa haitoshi baada ya kuunga-unga safari. Tulipofika Arusha, nilimtafutia guest ya bei rahisi na nikamlipia, niliona kama haamini hivi nilipomfungulia chumba na kumuaga kuwa asubuhi nampitia na kumuacha njia panda ya Karatu/ Babati (kesho yake nilikuwa naenda kwenye interview ya kaz Babatii).

Asubuhi yake nilimpitia guest na nikamchukua kwenye gari langu na tulipofika njiapanda ya Babati/Karatu nilimpandisha kwenye kifodi kilichokuwa kinaenda Karatu. Tuliendelea kuwasiliana kwa muda na akaniambia Karatu mambo hayakuwa mazuri na aliamua kurudi Mlandizi.

Mara ya pili nilikuwa natoka Kasulu kurudi Arusha kwa basi la Atraco lililokuwa linatoka Bujumbura- Dar. Niliketi na mama mmoja aliyekuwa na mtoto wa mgongoni wanatoka Burundi kwenda Arusha kama mimi. Tulifika Singida saa 5 hivi za usiku na basi lilikuwa linalala hapo ili asubuhi liendelee na safari ya Dar. Yule mama hakuwa mwenyeji pale Singida na nikamhakikishia kuwa tutatafuta guest na atakuwa salama. Tulihangaika guests kama mbili na tukapata vyumba viwili kwenye guest ya tatu. Nilimfungulia mlango wa chumba chake nikakikagua na kumuaga kuwa tutaonana asubuhi. Asubuhi nikamkuta yuko tayari na mtoto wake mgongoni tukaenda stendi na kupanda Bon City hadi Arusha ampapo tulimkuta mumewe, nami mke wangu amekuja kunipokea na tukatambulisha. Tuliendelea kuwasiliana kwa muda na baadaye mawasiliano yakakatika.

Kitu muhimu cha kujifunza hapa ni kuwa tujifunze kuwatendea mema wengine, tunapotendea mtu wema sio lazima tutangulize maslahi binafsi, ya kesho hayajulikani. Mtendee mtu kwa jinsi ileile ambayo ungependa mtu mwingine akutendee.

Vv
 
Hili jambo linawezekana kwa Mwanaume Jabali tu. Wavulana hawawezi kulala na mwanamke bila kumto...! Mwanamke unapoingia nae ndani anabet tu, ila anajua utamsumbua tu. Lakini nakuambia ukweli usipomgusa wala kuonesha uvulana, atakuheshimu sana. Utakuwa umeingia ktk kumbukumbu za maisha yake yote. Utakuwa rafiki yake Sana, hata siku ukimuomba atakupa bila usumbufu.

Hongera sana Kaka Umeonesha wewe ni Mwanaume Jabali.
 
Kutokana na hizi comment nimegundua wanaume wanapenda sana uzinzi duuh[emoji23][emoji23][emoji23]

Hongera kaka ulifanya kitu cha maana saana
 
Kutokana na hizi comment nimegundua wanaume wanapenda sana uzinzi duuh[emoji23][emoji23][emoji23]

Hongera kaka ulifanya kitu cha maana saana
Na wanawake wamegundua hivyo, ndiyo maana wakaja na majina "buzi" "kuchuna" na kuamua kufanya biashara ya maungo yao.

Vv
 
tamaa ikichukua amimba huzaa dhambi, hongera kwa kutokuwa na tamaa, Mwezako tamaa yangu imefanya leo hii nalea mimba ya miezi nane sehemu fulani
 
Wakati nimemaliza chuo kikuu nilipanga kagheto kangu mitaa fulani hivi huku mjini kwetu ili niweze kuwa karibu na harakati zangu za kuingiza vijisenti vya kujitegemea mjini. Miezi kama miwili walikuja mabinti kama nane hivi waliokuwa wanafanya field kwenye taasisi fulani hapo. Hawa walikua wanasoma certificate kwa hiyo walikua mabinti wadogo kabisa

Mabinti wale walionekana micharuko na watoto wa mjini isipokua mmoja tu ambaye alioneka wa kutoka kijijini au mshamba. Kutokana na mimi kuwa kijana pekee kwa ile nyumba kila binti alitaka ukaribu na mimi

Yule binti mshamba alinyanyaswa sana na wenzie kwa sababu walimwona haendani nao. Mimi huwa nina huruma na mabinti wanyonge hivyo nilimvuta karibu yangu. Alinizoea sana hasa kwa sababu nilimfariji kutokana na madhila ya wenzie

Nikitoka kwenye harakati zangu nlikua namletea ice cream,kinywaji au chips. Nikikosa kabisa angalau chungwa au pipi ikibidi

Hii iliwakasirisha hao watoto wa mjini mwishowe wakamtimua gheto kwa kusingizia kwamba ni mchafu (kiukweli hakuwa mchafu)

Basi alivyofukuzwa akanililia kwamba hana pa kwenda na hela ya kupanga chumba kujitegemea kwa sababu pale waliishi wanane chumba kimoja. Aliniomba aishi na mimi nikamkubalia kwa moyo mkunjufu. Kutokana na mazingira yenyewe,nilijiapiza kwamba sitatake advantage na kumlala mtoto wa watu kwa sababu ya matatizo yake

Basi tukaanza kuishi pamoja. Nampa pesa anaenda sokoni,anapika chakula kizuri sana,namnunulia muvi anaangalia,nikipata nguo ya bei rahisi nzuri namnunulia kama mwanangu

Tuliishi hivyo miezi miwili bila kupiga show kabisa. Muda wa kuoga na kuvaa tunapishana kupeana nafasi. Alikua akiniita kaka

Siku ya kuondoka ikawadia. Alinishukuru mno,alipiga magoti akalia machozi. Mimi poa nilitokwa na mchozi,sijui kwa sababu gani

Nilimtakia kila la heri naye akaniombea kila aina ya baraka. Aliondoka,tukawasiliana for few weeks tukapotezana. Sijui alipo kwa sasa ila naamini Mungu anaendelea kumpigania. Atakayemuoa yule binti atakua kapata mke bora kabisa!
 
daaa Big up sana kaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…