kijani11
JF-Expert Member
- Jan 19, 2014
- 8,113
- 8,610
Kuna wakati nilifikiri naweza hilo ila kwa sasa sijui kama nnaweza kujaribu hiyo kitu hata kidogo. Miezi miwili...!Wakati nimemaliza chuo kikuu nilipanga kagheto kangu mitaa fulani hivi huku mjini kwetu ili niweze kuwa karibu na harakati zangu za kuingiza vijisenti vya kujitegemea mjini. Miezi kama miwili walikuja mabinti kama nane hivi waliokuwa wanafanya field kwenye taasisi fulani hapo. Hawa walikua wanasoma certificate kwa hiyo walikua mabinti wadogo kabisa
Mabinti wale walionekana micharuko na watoto wa mjini isipokua mmoja tu ambaye alioneka wa kutoka kijijini au mshamba. Kutokana na mimi kuwa kijana pekee kwa ile nyumba kila binti alitaka ukaribu na mimi
Yule binti mshamba alinyanyaswa sana na wenzie kwa sababu walimwona haendani nao. Mimi huwa nina huruma na mabinti wanyonge hivyo nilimvuta karibu yangu. Alinizoea sana hasa kwa sababu nilimfariji kutokana na madhila ya wenzie
Nikitoka kwenye harakati zangu nlikua namletea ice cream,kinywaji au chips. Nikikosa kabisa angalau chungwa au pipi ikibidi
Hii iliwakasirisha hao watoto wa mjini mwishowe wakamtimua gheto kwa kusingizia kwamba ni mchafu (kiukweli hakuwa mchafu)
Basi alivyofukuzwa akanililia kwamba hana pa kwenda na hela ya kupanga chumba kujitegemea kwa sababu pale waliishi wanane chumba kimoja. Aliniomba aishi na mimi nikamkubalia kwa moyo mkunjufu. Kutokana na mazingira yenyewe,nilijiapiza kwamba sitatake advantage na kumlala mtoto wa watu kwa sababu ya matatizo yake
Basi tukaanza kuishi pamoja. Nampa pesa anaenda sokoni,anapika chakula kizuri sana,namnunulia muvi anaangalia,nikipata nguo ya bei rahisi nzuri namnunulia kama mwanangu
Tuliishi hivyo miezi miwili bila kupiga show kabisa. Muda wa kuoga na kuvaa tunapishana kupeana nafasi. Alikua akiniita kaka
Siku ya kuondoka ikawadia. Alinishukuru mno,alipiga magoti akalia machozi. Mimi poa nilitokwa na mchozi,sijui kwa sababu gani
Nilimtakia kila la heri naye akaniombea kila aina ya baraka. Aliondoka,tukawasiliana for few weeks tukapotezana. Sijui alipo kwa sasa ila naamini Mungu anaendelea kumpigania. Atakayemuoa yule binti atakua kapata mke bora kabisa!