Wale Wanasimba SC na wana Yanga SC mliokuwa 'mkinishambulia' JF nilipokuwa 'nikimsifia' Kibu Denis kuwa ni Hazina Kubwa mpo wapi leo?

Wale Wanasimba SC na wana Yanga SC mliokuwa 'mkinishambulia' JF nilipokuwa 'nikimsifia' Kibu Denis kuwa ni Hazina Kubwa mpo wapi leo?

Kudadadeki GENTAMYCINE sijawahi Kumpenda na Kumsifia Mchezaji Mbovu au Mchezaji ambaye hafanyi kile nilichomsifu nacho. Nikisema au Nikichambua huwa nakuwa nina uhakika kwani hata huo Mpira wenyewe naujua na isitoshe nimeucheza vile vile tena katika Ngazi zote Muhimu za awali Mashuleni, Mtaani, Wilayani na Mkoa pia enzi zangu ( zetu ) hizo.

Ni hapa hapa JamiiForums juzi katika moja ya Posts zangu Kumhusu Mchezaji Ousmane Papi Sakho na hata katika Uzi wangu mwingine Miezi kadhaa nilimsifia na Kumuelezea kwa Jicho la mbali, la Kiufundi na Kiubora Mchezaji Kibu Denis ila nikaambulia dhihaka na mpaka na Matusi vile vile.

Kauli yangu juu ya Mchezaji Kibu Denis kamwe haijawahi kubadilika na mara kwa mara nimekuwa nikisema kuwa huyu Mchezaji akijitambua, akkubali Kukosolewa, Kurekebishwa na kuongezewa Vitu vichache tu na Kocha Fundi na Mtaalam Pablo Franco basi hatokuwa tu ni Hazina Kubwa kwa Simba SC bali hata kwa Timu ya Taifa kwani ana Vitu vingi vizuri vya Mshambuliaji wa sasa na kupitia Yeye namuona Mbwana Samatta mpya na natabiri mapema kuwa Simba SC itatajiirika sana miaka Miwili ijayo kwa Kumuuza baada ya kutakiwa na Vilabu vikubwa na vya maana Afrika.

Mliokuwa mkinidhaki na kunitusi kwa Mimi Kumsifia Mchezaji Kibu Denis endeleeni kufanya hivyo, ila kama kuna Zawadi ya Kipekee kabisa ambayo Mwenyezi Mungu amenibariki nayo ( Kiumbaji ) ni kuwa na Jicho la Hatari na la Uhakika la Kuona mbali, Kuchambua na Kutathimini Jambo au Tukio lenye Uzito Kijamii.

Aliyemleta Kibu Denis Simba SC Asante.
Wacha wewe! Big Boss Popoma katika ubora wake!!
 
Kibu ni mchezaji ila so mzuri kiushndani, anacheza mipira ya ndondo nguvu nyingi akili kidogo, that's Y, anaweza kukokota mpira sanaa then akikutana na beki anayetumia akili Kariba ya Nondo & Inonga safari yake inaishia hapo na hatoi pass 'on/in time' yani mwenzake anafunguka muda sana ila jamaa anawavuta wapinzani hadi nafasi ya kupiga pass inakosekana
#Kibu akiweza kucheza mpira soft atatisha sana
Kwa mabeki wenye akili umekosea kumweka Nondo Mwamnyeto
 
Amepewa zawadi huko Dubai ya mchezaji bora wa siku
 
Nina wasi wasi na Jicho la mleta uzi isije kuwa anaona kwa jicho pendwa la wahuni mjini.
 
Kibu ni mchezaji mbovu, narudia tena Kibu ni mchezaji wa hovyo
 
Back
Top Bottom