Wale wote 'mnaomtetea' Haji Manara na 'Upuuzi' na 'Unafiki' wake popote pale mlipo naomba mnijibu haya Maswali yangu Kwenu

Wale wote 'mnaomtetea' Haji Manara na 'Upuuzi' na 'Unafiki' wake popote pale mlipo naomba mnijibu haya Maswali yangu Kwenu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
1. Je, Kisheria baada ya jana Haji Manara kuitaja Kampuni ya Azam akiihusisha kuwa na Vita ya Chuki na Kampuni za Mohammed Dewji yuko salama kama aliyeguswa akitaka Kumshtaki?

2. Je, kati ya aliyekuwa CEO Magori ambaye hakuwa kumpa Mkataba wowote Haji Manara na CEO Barbara ambaye kwa mwaka mzima alimpa Mkataba wa Milioni 4 kwa Mwezi ila akawa hataki nani ni Mzuri Kwake na nani alikuwa hamthamini?

3. Katika Sheria za Ajira na Miiko ya Kazi moja wapo ikiwa ni Kutokutoa Siri za Taasisi / Kampuni hivyo basi je, leo hii kwa Mambo ya Siri (ya ndani ya Menejimenti) ya Klabu aliyoyasema Haji Manara Simba SC ikiamua Kumshtaki Mahakamani atakuwa salama?

4. Je, kati ya Haji Manara ambaye amekiri kuwa amekaa Simba SC miaka Sita (6) bila kuwa na Mkataba huku akiridhika na Hali hiyo na Klabu ya Simba ambayo haikumpa huo Mkataba ni nani ni Mjinga (Ngumbaru) na Mpumbavu (Popoma ) hasa?

5. Haji Manara mara kwa mara amekuwa akisikika akiwadhihaki na akiwadharau Waandishi wa Habari akiwaita Takataka je, Haji Manara jana kaongea na Waandishi wa Habari Takataka au Waandishi wa Habari wa Kimataifa?

6. Je, ni kweli kuwa Haji Manara ndiyo Kainyanyua Simba SC Kiumaarufu tokea ianzishwe mwaka 1936 na kwamba Yeye ndiyo ana Thamani Kubwa kuliko Wazee wote wa Simba SC ambao tena wameifia Simba kwa kujitoa Mhanga ili aikute Simba SC hii aliyoikuta Yeye? Mfano Mzee Bamchawi na Wengineo.

7. Je, kwa tabia ya Umbea na Kuropoka aliyonayo Haji Manara mpaka ya Kutoa Siri za Taasisi na Kampuni unadhani kuna Vilabu vingine au Kampuni ( Corporates ) zingine leo hii zitathubutu kutaka Kufanya Kazi nae?

Ninayasubiri sana tu Majibu yenu hapa.
 
Acha umbea wewe. Kipindi anatukana watu hao simba si walikua wanafaurahia badala ya kumkanya, sasa tulieni kinyago mmekichonga wenyewe mbona mnalia lia?

Alafu huyo mropokaji yeye tatizo lake Barbara na MO sio SIMBA uelewe hili. Haijasema vibaya simba wala kuiponda kwasababu anaipenda SIMBA ila ana waandama ni hao wawili waliompiga vita
 
Mo anaitapeli vipi Simba?
Ndani ya miaka 4 anasema katoa bilion 21 CEO kamuweka yeye ofisi za simba zipo ofisini kwake operation za simba kwa asilimia kubwa zinafanywa kwa matakwa yake hesabu za simba haziko open alilalamika sportspesa wanalipa kidogo simba yeye anamatangazo zaidi ya moja kwenye jezi ya simba analipa ngapi gossip inasema haizidi million 200 yeye yupo sehemu ya uwekezaji anaamuaje kila kitu?

Peke yake wakati share ni 49 body ya simba anachagua yeye vikao vya body vinafanyika ofisini kwake huyu jamaa tukimchekea ipo siku ataondoka na simba itashindwa simama kama kampuni mashabiki wengi wamepagawa na form ambayo ni temporary tu tunataka timu hata form ikishuka ya uwanjani lakini financial simba isiteteleke
 
mwandishi hapa ndio kamaliza akili yote kwa hoja zilizojaa utumbo! 3 nayo ni hoja? ulisainishana wapi kuhusu kutoa siri za taasisi.. hii ina work endapo mtu unayemtuhumu ana mkataba na amesaini declaration of secrecy. unapoandika lazima ujue unachoandika lasivyo ni kuonyesha watu upeo mdogo ulio nao mbele ya jamii hii kubwa.
 
Sitaki kuamini utopolo leo wamesimama na Manara! Maisha yanaenda kasi sana aiseee! Mo tunajua ndio shida yenu,yaani maskini hapambani amfikie tajiri ila dua zake siku zote ni tajiri afilisike!

Hivi utopolo simba akishuka kiwango kwa kukosa udhamini mtafaidika nini? Uto hamuoni raha siku moja nchi inakuwa na vilabu giants nchini kuanzia kiuchumi hadi uwanjani?

Mfano misri kuna ahly,zamalek,pyramid nk,yaan ninyi mnaanzisha chokochoko simba iporomoke,akili za kijinga kabisa! Utopolo na wapenda mpira tunapaswa kukemea alichokifanya manara wadhamini au wawekezaji wataogopa kuwekeza ktk mpira wetu!
 
1. Je, Kisheria baada ya jana Haji Manara kuitaja Kampuni ya Azam akiihusisha kuwa na Vita ya Chuki na Kampuni za Mohammed Dewji yuko salama kama aliyeguswa akitaka Kumshtaki?...
Kwanza manara hajawahi kuwa mshabiki au mwanachama wa simba,huyo ni yanga pure kule alidata hela tu,na ndio maana yanga walikuja kwenye harusi yake na kumpa vitu vingi sana,

Pili hana mchango wowote kwa kuijenga simba,ni mpuuzi mtupu na kwa taarifa yako anahamia yanga,kuwa msemaji wao,kwa sasa yupo dubai eti anapumzika.

Mo asimhurumie ni lazima ampeleke mahakamani

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Shabiki yeyote wa simba mwenye akili timamu lazima asimame na Manara, bila shutuma za uongo dhidi yake sidhani kama Manara angefunguka, hata wewe ukisingiziwa jambo ili uwe huru ni lazima uuseme ukweli, tutamchukia bure Manara ila anayeivuruga simba ni mo na babra maana wanaoendesha taasisi as a family.
 
Back
Top Bottom