Haji kaongea vitu vingi ila tunaweza kuviganya sehemu mbili, ya kwanza kaongea kuhusu maslahi yake binafsi ambayo kiukweli hayatuhusu kama alikuwa analipwa au halipwi anatakiwa kujua wapi apeleke malalamiko yake. Swala la pili ameongea jinsi Mo anavyoitapeli Simba pale kuna hoja ambazo Simba wanatakiwa watoke wazijibu, kama Mo anaona Bhakresa anatoa pesa ndogo yeye anatakiwa atueleze mikataba anayoingia na Simba kutangaza bidhaa zake analipa shilingi ngapi?
Anasema kwa miaka 4 ametoa zaidi ya bilioni 21 mbona haelezi kuwa kipindi hicho Simba iliingiza shilingi ngapi na pia kwanini alikimbilia kuichukua asilimia 49 kabla mchakato haujakamilika.
Kwa mujibu wa makubaliano baada ya yeye kupitishwa kuwa mwekezaji alipaswa kulipa asilimia 10 mwezi wa kwanza na kumalizia nyingine baada ya miezi 3 je tukisema pesa alizopaswa kuwalipa Simba alikuwa anazifanyia biashara tutakuwa tumekosea.
Mo amesema mkataba wa Simba na Azam Tv hauendani na thamani ya Simba kama ni kweli atueleze bilioni 20 alizotoa kama asilimia 49 zinaendana na thamani ya Simba.
Sisi Simba tunachota ni kuwa na timu nzuri yenye mafanikio lakini asizuie watu wengine wanaotaka kuwekeza Simba.
Pia atueleze kama sheria zinataka wawekezaji wawe 3 kwanini ni yeye peke yake amepewa uwekezaji.