MOONFISH
Senior Member
- Jul 30, 2022
- 135
- 268
Habari wana jf kwanza kabisa nataka kusema mnisamehe kwa njia yoyote ile.
Mimi nilikuwa mpenzi sana wa BEER nimekunywa sana sio bia tu hadi MKALI yalio thhibitishwa na TBS.
Nimekunywa kwa miaka 12 mpaka sasa ila miaka 7 yote nilikuwa ni mzee wa makali sana na pia kuna mwaka nili wahi kunywa kwa siku 365 kila siku iendayo kwa mungu bila kupumzika.
Iko hivi nilikuwa kila mtu nikimuona mezani ameweka beer yoyote ya lite hasa hizi za kijani huwa nawadharau sana na kuona wanapoteza pesa kabisa.
Na huwa naona kama wanapoteza mda kabisa kwenye swala la burudani na nilikuwaa kila nikIona ME anakunywa hizo huwa sijui naona kama mshamba (NISEME BOYA) flani hivi ila akinywa manzi nilikuwa naona sawa maana nilikuwa na jua ni maji tu.
Beer ambayo mimi naipenda na nikiiona tu moyo unafanya paaaahhhh salala ni SAFARI LAGER aiseee yani kundi langu lote ilikuwa ni safari.
In short marafiki zangu wote vinywaji vyetu ilikuwa ni:
SAFARI
KONYAGI
VALUE
KIBO
THE KICK
BINGWA
PLISNER LAGER
N.K
Yani nikienda mahali nikikosa hizo basi ujue hatunywi tena beer na tukienda out na jamaa yoyte yule jua mezani hawezi tuwekea beer za lite kamwe.
Kwa utafiti wangu nimekuja kugundua kuwa mkali yananikataa kwa sasa, Maana zamani nilikuwa nakunywa naendelea na ishu zangu tena bapa kubwa na beer 1-2, nikinywa maji mengi kesho naamka fresh tu hata kama jana sijanywa maji. Ila kwa sasa nile au ninywe maji usiku ya kutosha asubuhi ni kama vile jana nilikuwa nalima au kupasuka kuni.
Kingine saizi nikinywa nashangaa nakuwa na mzuka kiasi kwamba nashindwa kujizuia nakuta natumia pesa ambayo sijapanga wakati sio kawaida nilikuwa nayo na kama kuna mziki naweza piga hip hop za BIG<2PAC<NAS<JAYZ<MEEK<ACE HOOD< mpaka kero.
Beer saizi nikinywa safari 3 naona naanza kulewa wakati zamani nilikuwa naanza kulewa baada ya kufika beer ya 5 au 6 au 7.
Kwa kitu ambachoo nimejaribu kubadilisha beer na mkali ila nimekundua kuwa kwa sasa nahitaji ku chilii kabisa maana mjini hizi fake naona zinataka kutu maliza maana sio kawaida na miaka kadha nyuma na mi hangover kama yote. Unakunywa K vant unapoteza kumbukumbu una kunywa value mzuka unapanda hadi unasahu kama ulikuja mpole mnyenyekevu, unakunywa beer moja mbili unajikuta kesho una buku.
Kuna siku nime sahau nikanywa beer nafika ya 4 naambiwa safari hamna zimeisha hakuna beer ni lite tu (nikamwambia dada hayo si maji tu). Nikamuuliza dada una kinywa gani akaniambia anachoo cha mkali 2500 (hii ni ndani ndani huko mkoa x porini nilikuwa) nikasema ngoja nipige short niende zangu home, akanimiminia kwenye glass aisee kumbe ni shimhaa bwana bwana!!!! hii kitu inapanda ndani ya sekunde iko kwa head ni sawa na double kick au cuca.
Nikajikuta mzuka una panda nikaongeza kengine nikasema hapa nisepe nikajua nikifika lodge nitakula nimeingia nasema nijipumzishe ndo nikalala nimekuja kuamkaa saa 8 mchanaa nimeenda toi narudi nimelala tena kumka saa 6 usiku khaaaa!!!! nikalala tena kumka saa 5 asubuhii sasa hapo mwili unadaii chakula na maji asikuambie mtu ni hatari na nusu.
Chakula kina goma ni maji maji nayo yaka goma kila nikiweka yanarudi nikiweka yanarudi aisee nimekuja kula kesho yake tena mara moja na ndo ukawa mwisho kabisa wa pombe ngumu maana mateso wanywaji na walevi wanayajua vizuri tu sema wengi hawasemi.
Sasa nimeamu rasmi kuwa nakunywa lite tu na ni beer ya srngt lite yani hata atokeee nani sigusi nimeanza taratibu kuizoea na kuangalia vizuri hangover ambayo bado sijaona, ila bado nasema ni beer safi ambayoo inaingia kichwani taratibu bila haraka na kutoka ni kwa haraka bila tatizo na unaweza fanya mambo yako bila kuvunja ratiba yoyote ile.
Wale wote mlio kuwa mna kunywa lite beer mnisamehe maana mwendo wa miaka yote umenichosha sasa ni miezi 9 sijagusa beer kali wala mkali. Saizi nikienda mahali nakuwa na uwezo wa ku budget vizuri nakuwa silewi ila nakuwa na enjoy mwili unakaa sawa na pia napata nafasi ya kuwa mimi kama mimi naweza kaa week mbili sina hata kiu wala hata ni kinywa huwa siwazi kesho, na kama nikisahau kula kwa bahati mbayaaa nakuwa sina neno. Saizii hadi marafiki naona wana nitania ila sio kesi mi ndo nimeamua na hata weekend ikitokea kikao bar hawaniiti tena maana wanajua nakunywa lite ila kwangu sio shida am happy.
NB: Kuna siku nilijaribu kuzigongaa lite nione kiwango chake aisee ni maji laki ikukweli kuna level unalewa ya kujijua na kufahamu kila kitu na keshoo una amka mweupe bila kujisikia halii yoyote mbaya.
Nawashauri wale wenye miaka kuanzia 13 kwenye gambe namaanisha wale wa gambe zito sio wa kuonjaaa itoshe kusema inatosha tupumzike kidogo.