Kilangi masanja
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 4,495
- 5,025
- Thread starter
-
- #3,401
Darasa safi ila tuende sambamba tujue
Kwenye offer kuna vitu vingi...
- Kwanza, bidhaa yenyewe inaweza kushuka bei kwa asilimia fulani.
-Pili, kwenye kila store wanatoa offer ya coupon ambazo ukinunua bidhaa iliyofikia kiwango fulani cha pesa unaweza kupata punguzo.
-Tatu, kuna AliExpress coupon, hizi unaweza uka add Kwenye bidhaa yeyote ile ukapata discount ilimradi tu iwe imefika kiwango cha thamani waliyoiweka.
-Nne, kuna promo code, ni code ambazo ukiziweka wakati wa ku check out unapata punguzo la asilimia fulani kwenye kila bidhaa iliyofikia kiwango fulani cha pesa.
-Jinsi ya kupata coupon; unaweza kupata kwa kubadilishana na coins, kupata kutoka kwa seller au kama rewad kwa kushiriki michezo mbalimbali inayosinamiwa na AliExpress.
-Kwa maana hiyo.. uki add hivyo vitu vyote wakati wa ku check out ndio unaweza kupata punguzo la hadi asilimia hamsini.
NB: Vyote vinaweza visitumike mara moja. Vigezo na masharti kuzingatiwa.