Hapana boss wangu. Kwanza tuelewane, si MediaTek SoC zote zinakuwa hazina nguvu.... Ebu chukulia mfano mwepesi tu "ni Tecno gani inayotumia ile chipset nzuri kabisa ya MediaTek?", jibu ni hakuna, hata hiyo Phantom 9 simu ya laki saba wameweka MediaTek Helio P35, unaikuta kwenye simu ya laki mbili na nusu ya Xiaomi Mi Play. Ni nani hapa apliwahi kutumia simu yenye MTK chipset zile za high-end kama Helio P60 au P70 akawa bored?!
Tukija kwenye upande wa Redmi Note 8 Pro ina MediaTek Helio G90T ni Chipset latest kabisa ya MTK na ipo vizuri sana hasa kwenye upande wa graphics imetengenezwa kwa HyperEngine technology ambayo itakuwa ina boost nguvu ya GPU na hivyo inazipita hata baadhi ya chipset za Snapdragon na Kirin Kwenye GPU. Kwa wale wapenzi wa video games hii ni simu mahususi kwaajili hiyo.