Wale wote wanaotumia bidhaa za kampuni ya Xiaomi tukutane hapa ili kupeana ujanja

Wale wote wanaotumia bidhaa za kampuni ya Xiaomi tukutane hapa ili kupeana ujanja

Hapana boss wangu. Kwanza tuelewane, si MediaTek SoC zote zinakuwa hazina nguvu.... Ebu chukulia mfano mwepesi tu "ni Tecno gani inayotumia ile chipset nzuri kabisa ya MediaTek?", jibu ni hakuna, hata hiyo Phantom 9 simu ya laki saba wameweka MediaTek Helio P35, unaikuta kwenye simu ya laki mbili na nusu ya Xiaomi Mi Play. Ni nani hapa apliwahi kutumia simu yenye MTK chipset zile za high-end kama Helio P60 au P70 akawa bored?!

Tukija kwenye upande wa Redmi Note 8 Pro ina MediaTek Helio G90T ni Chipset latest kabisa ya MTK na ipo vizuri sana hasa kwenye upande wa graphics imetengenezwa kwa HyperEngine technology ambayo itakuwa ina boost nguvu ya GPU na hivyo inazipita hata baadhi ya chipset za Snapdragon na Kirin Kwenye GPU. Kwa wale wapenzi wa video games hii ni simu mahususi kwaajili hiyo.
Shida hizi simu za MTK mara nyingi huwa hazipati update kama za snapdragon, nakumbuka kama redmi note 3 ile ya MTK ili stack kwenye lollipop wakati ile ya snapdragon ilipata marshmallow. Na GCAM nafikiri kwenye mtk haifanyi kazi. Mimi device za MTK huwa nazikimbia kabisa kutokana na hawa jamaa sio Developer friends.
 
Michele kwanza ikishindikana ndio kwa fundi.
Kuna redmi 5a dogo aliizamisha kwenye ndoo ya maji karibu nusu saa nzima na kitu kilizima kimoja but mchele ulifanya kazi yake kitu kinapiga mzigo mwaka sasa
Nimeweka jana kwa mchana kama masaa 10 hivi nimetoa inapiga kazi ila ina charge slowly tofauti na mwanzo naomba ushauri bado kabla sijapeleka kwa mafundi kuitia vidole.
 
Kumbuka ukiendeleea kuwasha sim yako wakat ina maji ndani utasababisha kupiga short kwenye circuit na kufanya sim isiwake tena......weka kwnye mchelee toa betry kabisa ......
Good.
Vp kwa non-removable bttry? Nako ni hivyo hivyo?
 
Wakuu mliopo Moshi, naomba kujua wapi napata fundi mzuri atakayeweza kufanya installation ya screen ya Redmi Note 6 Pro, msaada wa haraka tafadhali.
 
Wakuu mliopo Moshi, naomba kujua wapi napata fundi mzuri atakayeweza kufanya installation ya screen ya Redmi Note 6 Pro, msaada wa haraka tafadhali.
Hapo moshi stendi ndogo ( yan zinapopaki costa za arusha na hiace za sehem zingn) kuna geti la ushuru hapo, sasa mbele ya hilo geti la ushuru kuna supermarket inayotazamana na wewe ukiwa umesimama getini, ukivuka barabara tu kuelelea hiyo supermarket utatembea hatua 6 kushoto utamwona..ni fundi mzuri na anaaminika sana.

Au ukishashafika hapo geti la ushuru ( la stendi ndogo) muulize huyo aliyeko hapo getin akuonyeshe fundi simu aliyeko maeneno hayo (huyo fund ni shekhe) na atakuonyesha directly ofis yake ilipo mana inatazamana na yeye.
 
Ahsante sana mkuu kwa ushirikiano wako. Ni Rafiki Supermarket au?

Back
Top Bottom