Wale wote wanaotumia bidhaa za kampuni ya Xiaomi tukutane hapa ili kupeana ujanja

Wale wote wanaotumia bidhaa za kampuni ya Xiaomi tukutane hapa ili kupeana ujanja

Darasa safi ila tuende sambamba tujue
Kwenye offer kuna vitu vingi...
- Kwanza, bidhaa yenyewe inaweza kushuka bei kwa asilimia fulani.

-Pili, kwenye kila store wanatoa offer ya coupon ambazo ukinunua bidhaa iliyofikia kiwango fulani cha pesa unaweza kupata punguzo.

-Tatu, kuna AliExpress coupon, hizi unaweza uka add Kwenye bidhaa yeyote ile ukapata discount ilimradi tu iwe imefika kiwango cha thamani waliyoiweka.

-Nne, kuna promo code, ni code ambazo ukiziweka wakati wa ku check out unapata punguzo la asilimia fulani kwenye kila bidhaa iliyofikia kiwango fulani cha pesa.

-Jinsi ya kupata coupon; unaweza kupata kwa kubadilishana na coins, kupata kutoka kwa seller au kama rewad kwa kushiriki michezo mbalimbali inayosinamiwa na AliExpress.

-Kwa maana hiyo.. uki add hivyo vitu vyote wakati wa ku check out ndio unaweza kupata punguzo la hadi asilimia hamsini.

NB: Vyote vinaweza visitumike mara moja. Vigezo na masharti kuzingatiwa.
 
Kama nilivyotangulia kusema slow-motion video inachakatwa na Sensor ya camera. Na camera ya Redmi Note 6 Pro haifanyi kazi zaidi ya 60 FPS. Video za kawaida hurekodiwa kwa 30 FPS tu. Lakini slow-motion zinarekodiwa kwenye 60 FPS na hauwezi kuibadilisha, ndio sababu haipatikani kwenye setting.

Kwenye Redmi Note 6 Pro kuna baadhi ya apps zipo play store ambazo zitaweza kuweka hiyo slo motion effects pekee, unaweza search Slow-motion video zitakuja Apps nyingi tu za kuweka effects tu

Ila kwenye note 6 pro huwezi shoot hyp video mkuu? Au hata hiyo third part app ni ipi?
 
Andaa bajeti ya laki mbili na zaidi, hiyo screen yake ni Super Amoled
Mkuu,
Kwa mfano simu yako inatumia kioo cha lcd huwez replace na super amoled?

Tofauti kubwa kati ya amoled na lcd ni nn?

Hiv tofauti ya kiubora kwa simu zinazotumia exynos,heliokorin na snapdragon ni nn?
 
Wakuu msaada. Nataka kuagiza mzigo kutoka Aliexpress, najaza adress hapa, ila nimekwama hapo kwenye State/Province/Region. Anayejua cha kujaza hapo anaisaidie
 
Mkuu,
Kwa mfano simu yako inatumia kioo cha lcd huwez replace na super amoled?

Tofauti kubwa kati ya amoled na lcd ni nn?

Hiv tofauti ya kiubora kwa simu zinazotumia exynos,heliokorin na snapdragon ni nn?
Mkuu,
Kwa mfano simu yako inatumia kioo cha lcd huwez replace na super amoled?

Tofauti kubwa kati ya amoled na lcd ni nn?

Hiv tofauti ya kiubora kwa simu zinazotumia exynos,heliokorin na snapdragon ni nn?
Na mi nasubiri majibu
 
Mkuu,
Kwa mfano simu yako inatumia kioo cha lcd huwez replace na super amoled?

Tofauti kubwa kati ya amoled na lcd ni nn?

Hiv tofauti ya kiubora kwa simu zinazotumia exynos,heliokorin na snapdragon ni nn?

Smartphones hazijaundwa kufanyiwa upgrade hivyo hii replacement haiwezekani kufanyika. Kwa smartphones kadhaa za zamani zilikuwa zina matoleo yote mawili ya screen AMOLED na LCD kwahiyo ilikuwa inawezekana kufanya replacement.
Ila kwa upande wa pili kama unavyojua screen za AMOLED ni ghali sana hivyo kuna watengenezaji wa hizi screen wanatengeneza LCD screen endapo mtu atashindwa kumudu gharama za AMOLED screen pale simu yake ikipata damage na akashindwa kumudu gharama, ananunua na kuifunga LCD screen na itafanya kazi bila shida. Lakini kwa swali lako eti utoe LCD uweke AMOLED is highly unlikely to be possible!

Tofauti kubwa ya LCD screen inakuwa ina taa kwa nyuma ambazo ndio zinazalisha mwanga wa screen, wakati S-AMOLED screen inakuwa inazalisha mwanga yenyewe ndani ya screen. Hivyo inaifanya AMOLED screen kuwa ni more power efficient kuliko LCD screen inayotegemea taa kuzalisha mwanga.

Kwenye hizi Chipset za simu kuna kampuni inaitwa ARM ndio mtengenezaji, na baadae anauza technology yake kwa haya makampuni kama Qualcomm (Snapdragon) Samsung (Exynos), Huawei (Hisilicon), Apple. Halafu ndio wanaenda ku modify wao wenyewe wanavyotaka, kama kuongezewa speedi au uwezo wa graphics na kadhalika. Hivyo kila SoC ina pros & cons kutokana ni kipaumbele cha hiyo kampuni.

Nadhani utakuwa umepata uelewa kwa kiasi fulani.
 
vp kuhusu chipset ya mediatek
si itakuwa kama tecno flan hiv au infinix

Hapana boss wangu. Kwanza tuelewane, si MediaTek SoC zote zinakuwa hazina nguvu.... Ebu chukulia mfano mwepesi tu "ni Tecno gani inayotumia ile chipset nzuri kabisa ya MediaTek?", jibu ni hakuna, hata hiyo Phantom 9 simu ya laki saba wameweka MediaTek Helio P35, unaikuta kwenye simu ya laki mbili na nusu ya Xiaomi Mi Play. Ni nani hapa apliwahi kutumia simu yenye MTK chipset zile za high-end kama Helio P60 au P70 akawa bored?!

Tukija kwenye upande wa Redmi Note 8 Pro ina MediaTek Helio G90T ni Chipset latest kabisa ya MTK na ipo vizuri sana hasa kwenye upande wa graphics imetengenezwa kwa HyperEngine technology ambayo itakuwa ina boost nguvu ya GPU na hivyo inazipita hata baadhi ya chipset za Snapdragon na Kirin Kwenye GPU. Kwa wale wapenzi wa video games hii ni simu mahususi kwaajili hiyo.
 
Habari wakuu! Note 6 pro yangu imeingia Maji kwa chini huku kwenye Speaker haikuzama yote hivo imepelekea inawaka inazima inawaka inazima je fundi gani ni mzuri ambaye anaweza komaa nayo ikarudi kuwa poa! Ahsanteh
 
Fanya Huduma ya kwanza kwa kudisasembly then ivundike kwenye nusu kilo ya Michele kwa siku 4-7
Kumbuka kwamba parts zako zote unaiweka kwenye chombo chenye mfuniko usiopitisha hewa then mimi na Michele wa kutosha kuifukia alafu funga mfuniko iache humo kwa muda huo itatoka fresh tu
 
Habari wakuu! Note 6 pro yangu imeingia Maji kwa chini huku kwenye Speaker haikuzama yote hivo imepelekea inawaka inazima inawaka inazima je fundi gani ni mzuri ambaye anaweza komaa nayo ikarudi kuwa poa! Ahsanteh
Daah polee mkuu...kwakuwa upo Dar naamini itakuwa pouwa soon.
 
Back
Top Bottom