Wali kuku wa kukaanga

farkhina

Platinum Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
14,568
Reaction score
16,917
Mahitaji:

1.Mchele nusu kilo.

2.Kuku 1 kata vipande vipande...mroweke na tangawizi na chumvi.

3.Carrot 1 ikwangue.

4.Green peas/njegere kiasi.

5.Kitunguu kikubwa kimoja.

6.Mchanganyiko wa spices upendazo.

7.Kotmir au persley ukipenda.

8.Mafuta ya kupikia.

Namna ya kutaarisha:

Weka mafuta kiasi katika sufuria

Mkaange kuku hadi awe golden brown alafu mtoe weka pembeni.

Kaanga vitunguj maji kikikaribia kuwa brown weka peas na carrot wacha viwive kwa dakika 2-5.

Weka mchele changanya vizuri...weka kuku wako ulimkaanga na weka kotmir uliokata ndogo ndogo.

Punguzia moto weka maji kutokana na mchele wako na funika sufuria hadi kuwiva.

Kama haukauka vizuri weka katika oven au wekea mkaa juu.

Epua tayari kwa kuliwa.
 

Attachments

  • 1422156356876.jpg
    62 KB · Views: 1,597
  • 1422156384709.jpg
    63.6 KB · Views: 1,534
  • 1422156407361.jpg
    62.2 KB · Views: 1,556
  • 1422156427816.jpg
    74.6 KB · Views: 1,569
Hivi wapi nitapata mafunzo ata online ya mapishi ya kiafrika lakin yawe yameandikwa kwa english?
 
Ukhty Yaa Qammar..Hebu ntilie take-way 'angu nkale hukooo!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…