Wali kuku wa kukaanga

Wali kuku wa kukaanga

Habibty weee sivyo hivyo mpikie bwana kwanza umlishe yeye ashibe halafu ule weye au mlishane ati

Ha ha haaaaa. Asante mwaya. Hiyo ya kulishana tushaacha zamani, wacha turudishe mahaba ya awali. Lol
 
Mahitaji:

1.Mchele nusu kilo.

2.Kuku 1 kata vipande vipande...mroweke na tangawizi na chumvi.

3.Carrot 1 ikwangue.

4.Green peas/njegere kiasi.

5.Kitunguu kikubwa kimoja.

6.Mchanganyiko wa spices upendazo.

7.Kotmir au persley ukipenda.

8.Mafuta ya kupikia.

Namna ya kutaarisha:

Weka mafuta kiasi katika sufuria

Mkaange kuku hadi awe golden brown alafu mtoe weka pembeni.

Kaanga vitunguj maji kikikaribia kuwa brown weka peas na carrot wacha viwive kwa dakika 2-5.

Weka mchele changanya vizuri...weka kuku wako ulimkaanga na weka kotmir uliokata ndogo ndogo.

Punguzia moto weka maji kutokana na mchele wako na funika sufuria hadi kuwiva.

Kama haukauka vizuri weka katika oven au wekea mkaa juu.

Epua tayari kwa kuliwa.

Hivi dada umeolewa?
 
Hahahahah weee cheza tu utajuta wenzio tushashiba sahani nyeupe vitumbo mbwiiii

Hahahahaaaa pls nextime ukiona nachelewa nistue hata kwa pm, hasa pishi likiwa ni la vyakula bahari
 
Back
Top Bottom