Wali wa kitunguu

Wali wa kitunguu

Najua, lakini sasa unakulaje na vile vitunguu vilivyogeuka mkaa? Kasema hapo sio viive ni vinatakiwa kuungua ili kufanya wali uwe brown.
Unakua hivi,
Naweza kuiita 'Min Pilau'.
images%20(15).jpg
 
Hilo nalitambua, nimeamua tu kufanya masihara kufurahisha watu tuongeze siku za kuishi.

Lakini tukiweka utani pembeni kitunguu ni dawa hasa ukikitafuna kibichi. Tatizo harufu mdomoni, tena usiombe utafune kitunguu swaumu.
Kwa kweli umejua kunichekesha,

Yes kitunguu ni dawa sana na hata kwenye milo yetu ni vema kuweka vingi sio kitunguu kimoja kinakwatwa leo na kesho, lol,

Kitunguu swaumu nimekila sana kupunguza mwili (unfortunately umerudi tena kipindi hiki cha Corona, [emoji31])
 
Ni sababu ipi ya msingi inawafanya wapishi wakaange vitunguu hadi viungulie? Ile ni zaidi ya kuiva, haina madhara kiafya kweli? Inakua kama mkaa
Naomba ili swali akujibu Khantwe maana ye ndiyo amesemea kuunguza vitunguu, ila kwa mimi siunguzagi kabisa na pia sipendi maana kikishaungua tu ladha inabadilika na kuwa mbaya
 
Naomba ili swali akujibu Khantwe maana ye ndiyo amesemea kuunguza vitunguu, ila kwa mimi siunguzagi kabisa na pia sipendi maana kikishaungua tu ladha inabadilika na kuwa mbaya
Wahindi wanasema wali unakua mtamu tu wala hauiwi na ladha ya kuungua, kumbe Khantwe kagundua pishi matata,

images%20(14).jpg
 
Kwa kweli umejua kunichekesha,

Yes kitunguu ni dawa sana na hata kwenye milo yetu ni vema kuweka vingi sio kitunguu kimoja kinakwatwa leo na kesho, lol,

Kitunguu swaumu nimekila sana kupunguza mwili (unfortunately umerudi tena kipindi hiki cha Corona, [emoji31])

Siku mkienda tena kwenye vikao vya kugawiwa miili ( nyama) usinisahau kunipa mwaliko. Nna uhaba mkubwa sana. Sijai hata kwa kiganja
 
Siku mkienda tena kwenye vikao vya kugawiwa miili ( nyama) usinisahau kunipa mwaliko. Nna uhaba mkubwa sana. Sijai hata kwa kiganja
[emoji23][emoji23][emoji23],
Baki tu na hizo hizo kiduchu, me mwenyewe nazikataa wewe unazitaka za nini zinaleta mapresha na uvivu.
 
Kitunguu kina siri kubwa kwenye pishi lolote.. Hunogesha na kuleta ladha fulani very amazing

Jr[emoji769]
Mchuzi au pilau au kachumbari inoge lazima vitunguu viwe vingi hasa.
Huwa nawashangaa wanaopikia kitunguu nusu au kimoja ukitoa sababu za kiuchumi.
Hasa mchuzi wa nyama yoyote ili unoge vitunguu vingi.
 
Hilo nalitambua, nimeamua tu kufanya masihara kufurahisha watu tuongeze siku za kuishi.

Lakini tukiweka utani pembeni kitunguu ni dawa hasa ukikitafuna kibichi. Tatizo harufu mdomoni, tena usiombe utafune kitunguu swaumu.
Nilienda India na mgonjwa.
Hotel za kule kabla msosi haujaja unaletewa bakuli la vitunguu vibichi mtafune.
Ni kama starter wakati wa kusubiri main meal.
 
Hello guys,

Kwa wale wanaopenda kula kama mimi nimeona niwashirikishe hili pishi rahisi sana. Mwaka jana mwishoni katika kuhangaika na maisha nilienda mkoa mmoja ndanindani huko. Kule nilikuta wanapika wali wa kitunguu kwa kweli niliupenda. Pengine wengine mnajua ila nina uhakika wapo ambao hawafahamu. Twende pamoja.

1. Andaa kitunguu maji katakata vipande vya kawaida.

2. Tia mafuta kwenye sufuria unayotaka kupikia wali (hakikisha umeandaa maji ya moto pembeni).

3. Tia vitunguu kwenye mafuta yaliyochemka, kaanga mpaka viungue (sio viive, vinatakiwa viungue).

4. Tia mchele, geuza hadi vitunguu vichanganyike na vitunguu (mchele ubadilike rangi). Baada ya hapo tia maji na endelea na hatua zingine kama kawaida.

Wali unakuwa na ladha fulani hivi ya kuvutia, mimi niliupenda najua na wewe utaupenda

Huu wali kuna mtu wangu wa karibu ndiyo wali wake, mtamu sana!

Tatizo umenikataa, nikiula lazima niharishe sana na kuumwa tumbo! Nimejaribu mara kadhaa hali ni hiyo hiyo, sijui kwa nini hapo!
 
Back
Top Bottom