Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,926
- 17,030
Jamaa yangu tupo naye kazini kitambo sana. Si haba vijicent vipo. Shida kubwa ya jamaa ni ubabe na unyanyasaji sababu ya vijicent.
Huwa namwambia asiwe na lugha za kibabe, dharau na unyanyasaji kwa watu wa kipato cha chini. Haelewi.
Anajenga nyumba. Ashafukuza sana mafundi bila kuwalipa na matusi mengi akitishia kuwaweka ndani n.k ni jambo la kawaida kumsikia akiwaambia umaskini wenu na kukosa akili ndo kumewafanya mchague hii kazi.
Basi amejenga nyumba yake akiwalalia sana mafundi ...sana yaani kumbe nao wanajua pa kumlalia.
Leo tumeenda akakague mifumo ya maji baada ya kuunganishwa mabomba...aiseee.... Alikuwa kila akifungua bomba maji yanatokea ukutani...kumbe katika hali ya kumkomoa mafundi walikuwa wanaweka mabomba hawafikishi mwisho.
Kwa hiyo ameenda kufungua maji kwenye koki kuu...kuingia ndani anakuta kuta zinatiririsha maji tu...
Hivyo anapaswa abomoe afunge mabomba upya...Kuta zinatiririsha maji ile mbaya. Mimi kwenda gusa zaidi zile kuta aisee ....hazifai.
Yaani ukipata muda ukaanza ukuna au tekenya ukuta mchanga unamiminika chini hadi ukuta unatoboka.
Ile nyumba ina maeneo ukikaa tu kama upo idle kwa kidole tu anza kufanya kama unaukuna ukuta au fanya kama una utekenya ukuta unacheka kinyama.
Mafundi haijulikani wanakaa wapi ila nao wameshalipiza wameondoka zao.ukijua ya mbele wenzio wanajua ya nyuma.