KERO Walimu ajira mpya Halmashauri ya Mkalama tumelipwa TZS 250,000 badala ya 925,000

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi walimu walioajiriwa mwezi Januari 2026 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Singida, tunaomba mamlaka husika zisaidie kufuatilia stahiki zetu za fedha za kujikimu ambazo tumekuwa tukizidai kwa muda mrefu.

Tumekuwa tukipewa taarifa kwamba fedha hizo bado hazijafika. Hata hivyo, hivi karibuni tulilipwa TSh 250,000/= kila mmoja, bila kupewa maelezo ya wazi kuhusu hesabu ya malipo hayo na stahiki zetu zote.

Tunaomba TAMISEMI, TSC, Ofisi ya Rais–Utumishi na mamlaka nyingine husika kuingilia kati, kutupatia ufafanuzi wa maandishi kuhusu malipo hayo na kuhakikisha tunalipwa stahiki zetu zote kwa mujibu wa sheria na taratibu.

Tunaomba haki yetu, si upendeleo.
 
Mwalimu jitahidi kupoga hoja kila wazo weka kwenye aya ya peke yake .

Hujafafanua yafuatayo juu ya madai yako;

1; Allowance unafaa kilipwa kiasi gani?
2: Ngazi ya kiwanga cha mshara wako na malipo hayo yalifanyika vip ( bank au cash)
3: Je , kiongozi umejaribu kuwasiliana nae- mwl mkuu , mrabibu au afisa elimu .

Nb ; UANDISHI WAKO UTIA MASHAKA

Anyway pole mwalimu
 
KWA KAWAIDA HIZO PESA SI HUWA MNAPEWA KILA MMOJA KUTOKANA NA SIFA ALIZONAZO, AU WALIOSINGO NA WALIO NA NDOA HUWA WANALIPWA PESA YA KUJIKIMU INAYOFANANA ?
Hela ya kujikimu inabidi ilipwe sawa kwa kila mtumishi mpya, kwa sababu wote wanaenda kuazisha maisha upya, lakini imekuwa tofauti kidogo kwa sasa wanalipwa kulingana na kiwango cha elimu yake
 
Mimi nachojua mwenye ndoa na asiye na ndoa wanalipwa viwango tofauti kulingana mwongozo uliopo.
 
We unachanganya, hela ya uhamisho kutoka kituo A kwenda kituo B (Disturbancee allowance and Ground Transport), hii ndo hulipwa kulingana na ukubwa wa familia yako.

Hela ya kujikimu inabidi ilipwe kabla hata kazi haujaaza ili ikusaidie kuweka mazingira safi sehemu utakayoenda kufikia kwenye kituo chako kipya.
 
Sawa
 
Zingatia CV yako yakuombea kazi mwalimu. Hukueleza uwezo wako wakutatua changamoto na kuhandle pressure ukiwa kazini? Kama ulieleza, kuweka mambo ya kazini mitandaoni ni hatua ya ngapi baada ya zingine kushindikana?
 
Wewe ni mpumbavu
 
Walimu hua hamuishi kulialia tu ajira uliomba ya nini mkikosa ajira mnalia mkipata mnanilia sasa msaidiweje mshahara hulipwi? Uliomba ajira ya nn acha kazi
 
Sisi walimu walioajiriwa mwezi Januari 2026 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Singida, tunaomba mamlaka husika zisaidie kufuatilia stahiki zetu za fedha za kujikimu ambazo tumekuwa tukizidai kwa muda mrefu.

Tumekuwa tukipewa taarifa kwamba fedha hizo bado hazijafika. Hata hivyo, hivi karibuni tulilipwa TSh 250,000/= kila mmoja, bila kupewa maelezo ya wazi kuhusu hesabu ya malipo hayo na stahiki zetu zote.

Tunaomba TAMISEMI, TSC, Ofisi ya Rais–Utumishi na mamlaka nyingine husika kuingilia kati, kutupatia ufafanuzi wa maandishi kuhusu malipo hayo na kuhakikisha tunalipwa stahiki zetu zote kwa mujibu wa sheria na taratibu.

Tunaomba haki yetu, si upendeleo.

Ila TAMISEMI AISEEEE
 
Ili ionakane tumeajiri watu wengi
 
Watu wajinga kweli, hivi hujuwi unaposema tamisemi ndo huyo huyo halmashauri?, halmashauri ni mtendaji wa tamisemi, ni sawa na kkusema vituo vya polisi kupokea maelekezo ya wizara ya mambo ya ndani,
 
Back
Top Bottom