Walimu kuajiriwa na TSC badala ya Wizara kunaenda kutengeneza rushwa, undugu na kujuana kwenye ajira. Rais litazame hili linaenda kukuharibia

Ninadhani wahusika wamesikia changamoto za utaratibu mpya,lakini tuwape "benefit of doubt " waanze utekelezaji wakikwama watarekebisha utaratibu.
Si vema kuhukumu kuwa huko halmashauri za wilaya rushwa na upendeleo umetamalaki,kiasi kwamba watendaji wote wilayani wataleta ndugu zao au watapokea rushwa kuleta watu wao.
Kwa uelewa wangu, wilayani Kuna Takukuru na Usalama wa Taifa ambao wako Kyle kuhakikisha kuwa haki inatendeka na taifa linakuwa salama.

Ushauri wangu
1). Maombi yatumwe kwenye hizo tume za Walimu za wilaya kupitia mfumo wa ki Electronics.
2). wakati wa kupanga ajira ,hizi tume zishirikishe tukukuru na TISS.
3).Tamisemi iwe inatoa vigezo na miongozo ya uendeshaji wa zoezi zima.
4).Tume itakayobainika kukosa maadili ya kazi zao iwajibike Mara moja.

Manufaa ya utaratibu mpya
1).Walimu wengi watapangiwa kazi maeneo waliyoombea kazi
2).Tume ya Walimu ya Wilaya husika itakuwa inafahamu mahitaji halisi ya Walimu kwa kila shule wilayani
3). Utaratibu wa kuajiri Walimu kutoka Makao Makuu Tamisemi,mara ya mwisho,ulisababisha Mwalimu mmoja jina lake kujirudia mara 196,(unapokuwa na idadi kubwa ya Waombaji na watalaam wa IT wasio na weledi).
4). wilaya za pembezoni,nazo zitapata Walimu waliokubaliana na mazingira ya eneo hilo (itaondosha walimu wengi kutoripoti vituo vya kazi au kuomba uhamisho ndani ya muda mfupi)
 
Rushwa ipo siku nyingi huko TAMISEMI
 
Miaka 50 nyuma
 
Huu utaratibu sio kwamba ni mpya uliwahi kuwepo miaka ya nyuma japo kwa kipindi hicho ulisimamiwa na wakurugenzi wa halmashauri. Rushwa ikawa inatembea balaa na ukitaka kupangiwa mjini unatoa hela kazi inakwisha na hii ndio ilichangia shule za mjini kuwa na walimu wengi kuliko za vijijini. Baada ya kuliona hilo serikali ikafuta huo utaratibu wa ajira ukarudishwa kuwa chini ya wizara. Kwahiyo kusema wapewe muda ni kubariki uhuni uliofanyika miaka ya nyuma kuendelea kuwatafuna watanzania. Hili halikubaliki
 
Rushwa ipo siku nyingi huko TAMISEMI
Ni kweli ipo lakini mfumo wa kielektroniki unaotumika sasa umesaidia kupunguzwa rushwa na kujuana kwenye ajira kwa kiwango kikubwa huwezi kufananisha na rushwa itakayotembea endapo utaratibu utakuwa chini ya TSC
 
Viongozi wa ccm huwa wanatumia kila namna kutengeneza mazingira ya rushwa ili wanufaike nayo binafsi.
 
Wewe utakuwa ni mtumishi wa hiyo tume thus why unatetea ili upate nafasi ya kuchomeka ndugu zako kwenye ajira!
 
eti rais!

haya malamiko yenu yapelekeni kwa mkwe wake ndiyo yupo incharge.
 
Hata Sasa hivi bado inasemekana ajira zinatolewa Kwa kujuana...

Hakuna jipya pambana...
 
Kwanini tuogope kabla... Wacha wajaribu kwanza.
 
Ofisi za tsc zinanuka rushwa za kila aina.. ukiwa mwanaume pesa ndo pona yako na ukiwa mwanamke rushwa ya ngono itakuhusu. Makatibu wa TSc wilaya wamejitunuku Umungu mtu! Ummy aliekushauri amekupotosha!
 
Kwanini tuogope kabla... Wacha wajaribu kwanza.
Sio geni lilikuwepo na hali ilikuwa mbaya zaidi ndipo serikali ikarudisha utaratibu wa kuajiri wizarani. Sasa ukiona linataka kurudishwa tena ujue wapiga madili wamerudi kazini
 
Ofisi za tsc zinanuka rushwa za kila aina.. ukiwa mwanaume pesa ndo pona yako na ukiwa mwanamke rushwa ya ngono itakuhusu. Makatibu wa TSc wilaya wamejitunuku Umungu mtu! Ummy aliekushauri amekupotosha!
Huyu waziri kabla ya kufikia huu uamzi angefanya japo research kwa walimu kuona namna gani masuala yao ya kinadhamu yanavyoshughuliwa na hawa TSC. Ni rushwa tupu.

Tena hawa kisheria hawana mamlaka ya kuajiri ila kwakuwa ni wapiga dili ndio watakuwa wamemshauri waziri awapatie kibali cha kuajiri na waziri naye bila kufikiri akajaa mzima mzima
 
Kwani nani kasema njia ya kietronic haiwezi kutumika na TSC?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…