WALIMU: Kwa wale wanaotaka kubadilishana vituo vya kazi
 
Njoo sengerema nije Misungwi mwalimu shule ya msingi.
 
Njoo Karagwe Kagera, nije wilaya yoyote katika mikoa ya Singida, Manyara, Arusha, Dodoma, Au Morogoro, idara Msingi
 
Mimi nakushauri ufuate tu utaratibu uliowekwa. Kinyume na hapo, jiandae kutapeliwa.
Kama huna mtu wa kubadilishana naye; andika barua ya kuomba uhamisho yenye anuani 5 pale juu kushoto.

Anuani ya Mkurugenzi wa kule unakoenda iwe juu kabisa, inafuatiwa na ya Afisa elimu unakokwenda, halafu Mkurugenzi wa Halmashauri yako, Afisa elimu wako, na chini kabisa iwe ya mkuu wako wa shule. Na wote hao wanatakiwa kukupitishia hiyo barua.

Ambatanisha pia nakala zifuatazo; Barua yako ya ajira, barua ya kuthibitishwa kazini, na kitambulisho chako cha kazi.

Wakikusainia hao wote, andika sasa covering letter ya huo umaisho wako na uipeleke Tamisemi ukiambatanisha na hiyo barua uliyo sainiwa. NB:- lazima uwe na sababu za msingi za kuhama ndugu mwalimu.
Mkuu barikiwa Sana ila Kuna jambo naomba ufafanuzi wa kina Zaidi Barua yenye sababu za Msingi ni hii ya kwanza, covering letter or zote mbili?
 
Mkuu barikiwa Sana ila Kuna jambo naomba ufafanuzi wa kina Zaidi Barua yenye sababu za Msingi ni hii ya kwanza, covering letter or zote mbili?
Viambatanisho kuhusu sababu zako za kuhama ndiyo unaambatanisha. Ila na hiyo barua yenye anuani 5 ndiyo hiyo ya kwanza.
 
Back
Top Bottom