Kwanza niulize, hizo m 200 unamaanisha uwekezaji wake au m 200 zilizopo kwenye akaunti. Mpwayungu hao walimu waliopigika wako huko dar.. njoo vijijini huku kuna mwl yuko huku ana ng'ombe 1500, semi trailer moja na shamba la miti viberiti lenye miti 78,000 crdb walishamtembelea sana anawapiga chini kwa bei yao ndogo (naomba nisifungue code zake nyingi labda yuko humu)..
Sasa kuna walimu wengine huku kwetu wana vigest, maduka ya vifaa vya ujenzi, vigari vya passos, vitz kawaida tu nisijue akaunti zao zikoje.
Pia wapo wengine tulionao huku ambao tunawachukulia kuwa ni maskini tu ambao wewe ndio unawaona huko dar wana pikipiki boxer moja ya kwendea kazini, ana kanyumba kake hajapanga na ka shamba ka ekari tatu au mbili ka kulima mazao chakula ili kumaliza mwaka (we mpwayungu sijui ni kaka au dada maana ulitamani kuwa mwanamke unapotoa hoja za vipato vya walimu tunakucheki tu)
Ha ha huku tuna mwl ana miliki gereji, mashine za kusaga sasa ni utitiri.