kingunge wa jf
JF-Expert Member
- Dec 24, 2013
- 464
- 447
Hili ni jambo la kusikitisha sana baada ya waalimu mkoani Mwanza kufanya mafunzo ya mtaala mpya bila Posho ya kujikimu wakiwa mafunzoni.
Fikiria serikali inatekeleza jambo kubwa kama hili halafu unamtoa Mwalimu nje ya kituo chake cha kazj anahudhuria seminar bila Allawance yeyote?
Kwa nini idara ya Afya na idara zingine kama kuna mafunzo nje ya kituo cha kazi huwa wanalipwa posho lakini hili halipo kwa waalimu? Au Sheria za utumishi wa umma haziwahusu walimu?
Kwa nini serikali inathamini walimu kipindi cha uchaguzi tu na sio kwenye kazi za msingi kwa taifa?
Inawezekanaje unamtoa mwalimu nje ya kutuo chake cha kazi unaenda kumpa mafunzo bila kupata chochote.
Walimu badilikeni hizi dharau mnazooneshwa na serikali yenu mnapaswa kukomesha. Fikirieni mnazidiwa mpaka na watu wa kawaida kabisa, mkulima anahudhuria mafunzo lakini anapata posho ila sio mwalimu. Hii sio sawa hata kidogo.