DOKEZO Walimu Mkoani Mwanza wafanya Mafunzo ya Mtaala Mpya bila Posho

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hivi wanawachukuliaje hao watumishi?
Nawashauri wawachangishe fedha za masomo ya ziada, huko watapata viposho kdg. Serikalini wasahau
 
Nchi hii ni ya kipumbavu sana.

Huo mtaala mpya walipewa semina watu wote mashuhuri wakiwemo mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa na wilaya, wakurugenzi na kula posho zao mlima zikiwemo on transit, perdiem na allowance zingine.

Ila Kwa WALIMU sasa wengine wamepewa buku 3 ya Chai. Na hawa WALIMU ndio watekelezaji wakubwa wa huo mtaala...
Watayaona majibu yake
 
Fikiria serikali inatekeleza jambo kubwa kama hili halafu unamtoa Mwalimu nje ya kituo chake cha kazj anahudhuria seminar bila Allawance yeyote?

Kwa nini idara ya Afya na idara zingine kama kuna mafunzo nje ya kituo cha kazi huwa wanalipwa posho lakini hili halipo kwa waalimu? Au Sheria za utumishi wa umma haziwahusu walimu?
Kumbukeni ninyi ndiyo washangiliaji namba moja kwenye ushindi wa kishindo
 
Hivi ndo huo mtaala nasikia watu wanalalamika kuwa Mambo ya baleghe yamepelekwa darasa la nne!
Sasa mwl kuelezea mtoto wa la nne habari za kubaleghe nao hawajafikia watawaelewa kweli!
Na watoto wa sasa hivi wanasoma wakiwa wadogo.

Nafikiri pia wameangalia mabadiliko na mtindo wa maisha wa sasa.

Kasi ya kunjunjana watoto wa siku hizi, vidogo vinaanza kuhenyesha via vya uzazi.
 
Hili ni jambo la kusikitisha sana baada ya waalimu mkoani Mwanza kufanya mafunzo ya mtaala mpya bila Posho ya kujikimu wakiwa mafunzoni.

Fikiria serikali inatekeleza jambo kubwa kama hili halafu unamtoa Mwalimu nje ya kituo chake cha kazj anahudhuria seminar bila Allawance yeyote?

Kwa nini idara ya Afya na idara zingine kama kuna mafunzo nje ya kituo cha kazi huwa wanalipwa posho lakini hili halipo kwa waalimu? Au Sheria za utumishi wa umma haziwahusu walimu?

Kwa nini serikali inathamini walimu kipindi cha uchaguzi tu na sio kwenye kazi za msingi kwa taifa?
Inawezekanaje unamtoa mwalimu nje ya kutuo chake cha kazi unaenda kumpa mafunzo bila kupata chochote.

Walimu badilikeni hizi dharau mnazooneshwa na serikali yenu mnapaswa kukomesha. Fikirieni mnazidiwa mpaka na watu wa kawaida kabisa, mkulima anahudhuria mafunzo lakini anapata posho ila sio mwalimu. Hii sio sawa hata kidogo.
aisee kumbe wale waliopewa Afu tatu wana unafuu

cc LIKUD
 
Vpi somo la uchumi/ biashara wameliweka...??

Walimu na policcm ni kimbilio la waliofeli... by roma
 
Poleni Sana walimu, tatizo nyie watu mmefanywa backup ya sere Kali ya njano kwahiyo wanawamudu hata mkilalamika. Mkishavaa Yale matisheti na kofia basi kijani daima
 
mkulima anahudhuria mafunzo lakini anapata posho ila sio mwalimu
Hii nikweli huwa tukienda maonyesho huwa tunalipwa na halimashauri 600k kwa siku zote tutakazo kaa huko tukichuliwa na mgodi ni mara mbili yake hapoa bado chakula na kulala ni wao wanatafuta na usalama juu ukiumwa wao
 
Hili ni jambo la kusikitisha sana baada ya waalimu mkoani Mwanza kufanya mafunzo ya mtaala mpya bila Posho ya kujikimu wakiwa mafunzoni.

Fikiria serikali inatekeleza jambo kubwa kama hili halafu unamtoa Mwalimu nje ya kituo chake cha kazj anahudhuria seminar bila Allawance yeyote?

Kwa nini idara ya Afya na idara zingine kama kuna mafunzo nje ya kituo cha kazi huwa wanalipwa posho lakini hili halipo kwa waalimu? Au Sheria za utumishi wa umma haziwahusu walimu?

Kwa nini serikali inathamini walimu kipindi cha uchaguzi tu na sio kwenye kazi za msingi kwa taifa?
Inawezekanaje unamtoa mwalimu nje ya kutuo chake cha kazi unaenda kumpa mafunzo bila kupata chochote.

Walimu badilikeni hizi dharau mnazooneshwa na serikali yenu mnapaswa kukomesha. Fikirieni mnazidiwa mpaka na watu wa kawaida kabisa, mkulima anahudhuria mafunzo lakini anapata posho ila sio mwalimu. Hii sio sawa hata kidogo.
Sio mwanza tu nafikiri ni mikoa yote maana hata sie tumetoka juzi tu hakuna cha posho wala nauri Tz elimu sio kipaumbele chake
 
Back
Top Bottom