DOKEZO Walimu Mkoani Mwanza wafanya Mafunzo ya Mtaala Mpya bila Posho

DOKEZO Walimu Mkoani Mwanza wafanya Mafunzo ya Mtaala Mpya bila Posho

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ni kauli ya kutolewa na layman na si msomi. Kama uliweza kutoa pesa za elimu bure from primary to advanced level utakuwa unahudumia watu kiasi gani? Iweje kwa watumishi 300,000 ndo iwe kubwa kwa issue inayotokea mara 1 baada ya miaka?? Na bado si walimu wote wanaohusika na hayo mafunzo ni wale watakaofundisha kidato cha kwanza tu
Mwalimu punguza wenge. Kupanga ni kuchagua ulichagua mwenyewe ualimu
 
Mwalimu punguza wenge. Kupanga ni kuchagua ulichagua mwenyewe ualimu
Kwani wenyewe kuweka kulipwa ikiwa utaenda kikazi nje ya kituo walilazimishwa? Naweza nisiwe mwl lakini haimaanishi kisa siyo ndo nione na uonevu kwao ni sahihi.
 
Maalimu ni majinga sana yanapelekeshwa tu, na hapo uone ni nchi nzima na yanakubali tu uoga
 
Hili ni jambo la kusikitisha sana baada ya waalimu mkoani Mwanza kufanya mafunzo ya mtaala mpya bila Posho ya kujikimu wakiwa mafunzoni.

Fikiria serikali inatekeleza jambo kubwa kama hili halafu unamtoa Mwalimu nje ya kituo chake cha kazj anahudhuria seminar bila Allawance yeyote?

Kwa nini idara ya Afya na idara zingine kama kuna mafunzo nje ya kituo cha kazi huwa wanalipwa posho lakini hili halipo kwa waalimu? Au Sheria za utumishi wa umma haziwahusu walimu?

Kwa nini serikali inathamini walimu kipindi cha uchaguzi tu na sio kwenye kazi za msingi kwa taifa?
Inawezekanaje unamtoa mwalimu nje ya kutuo chake cha kazi unaenda kumpa mafunzo bila kupata chochote.

Walimu badilikeni hizi dharau mnazooneshwa na serikali yenu mnapaswa kukomesha. Fikirieni mnazidiwa mpaka na watu wa kawaida kabisa, mkulima anahudhuria mafunzo lakini anapata posho ila sio mwalimu. Hii sio sawa hata kidogo.
Si ndo uzalendo kwa Taifa lenu? Acheni Njaa, Tangulieni Utaifa Mbele
 
Back
Top Bottom