Wito na Uzalendo iwe kwa walimu tu? Kila mmoja katika nchi anatakiwa kuwa mzalendo. Sio kunyonya watu wachache na kuwapa maneno ya ulaghai kuwa wawe Wazalendo wakati katika nchi ileile kuna watu wana neema utadhani ni nchi mbili tofauti. Sio walimu tu, watumishi wengi wa umma wanaishi maisha below the standard. Wengi wao hawawezi ku-afford hata bills za kawaida kabisa za kila mwezi licha ya kuwa na ajira. Kila siku unaambiwa kuna tume imeundwa sijui kufuatilia mishahara, sijui michakato, sijui nini na nini. Unyonyaji mtupu na usanii sanii mwingi. Mtu mwenye ngozi nyeusi ni kiumbe cha ajabu kabisa. Inakera sana wakati mwingine na inabidi hata kutumia maneno makali.
Nchi za wenzetu wanajitahidi ku-standardize vipato vya raia wake ila sie tunakomea kusababisha kuwepo kwa gap kubwa kati la wenye nacho na la wasio nacho kwa kisingizio cha umaskini wa kutengenezwa unaoweza kuepukika kabisa.
Mie nawashauri walimu na watumishi wengine hasa ambao ndio wameanza ajira zao kuweka kipaumbele suala la ufugaji angalau Ng'ombe wa maziwa na kuku wa nyama au mayai iwe kipaumbele kikubwa zaidi kuliko mambo mengine yoyote yale. Kuliko sijui ku-plan kuoa au kuolewa, au kujenga nyumba, fanya juu chini kuhakikisha unapata elimu sahihi ya ufugaji kisha uhakikishe nyumbani kwako unafuga Ng'ombe wa maziwa na kuku ili kuepukana na fedheha za malipo duni kabisa ya wenye mamalaka wanaofanya maksudi kuwaletea umaskini watu wake.