Wana Jf mimi ni mmoja wa wazazi wa watoto ktk shule ya mchepuo wa kiingereza ya serikali iliyopo Upanga Mashariki Diamond Primary School,shule hii ada tunalipa shs 400,000/= kwa mwaka na ni utaratibu kila muhula tunalipa shs 200,000/= ila ajabu ni kua shule imefunguliwa juzi June 6 ila mtt wangu na wengine tayari wamenyanganywa mabegi na kutengwa darasani et kisa hawajalipa ada ya muhula wa pili
Inashangaza sana jinsi uongozi wa shule hii unavyowatendea watoto wetu sababu ata kama mtt alikua anakuaa dawati za mbele wamerudishwa nyuma kabisa na kutengwa na wenzao kisa tu ada ya muhula wa pili haijalipwa ilhali shule zenyewe zimefunguliwa juzi tu,,sasa naombeni tusaidiane hapa kujua n wapi wametoa haki ya kuwabagua watoto ilhali shule ni ya serikali na katiba yetu inapinga aina yoyote ya ubaguzi katika nchi hii!
Naomba kuwasilisha!