Walimu naomba mjirekebishe na hili la kuomba tip

Walimu naomba mjirekebishe na hili la kuomba tip

🤣🤣🤣🤣
Hii haituhusu, wazazi wetu ni walalahoi kama sisi tu.
Ni wale wanataka rusha ngumi kwa kikao kisa wameambiwa remedial itakua ni tsh 200 😹😹😹😹😹
 
Kwanini uwajumuishe wote na wa serikali.

Serikalin kuna maadili. Hiyo haiwahusu government teachers kaa mbali wewe kiazi maani.na zako


Tena edit uzi wako
Mkuu angekuwa specific na shule x. Hata huko private Kuna walimu wako simati.Mleta nada anasomesha mtoto wake kwenye shule ya kuunga unga hata kulipa walimu ni shida. By the way Hilo laweza kuwa tatizo la mtu MMOJA ila yeye anajumuisha walimu wote.
 
Mkiambiwa mtoe michango mnalalamika, mkiombwa kwa wema bado lawama.
Si kakuomba kwani umelazimishwa kumpa??
 
Imekuwa kawaida sana kwa walimu kuanzia chekechea, sekondari kasoro labda vyuoni tu. kupenda sana kuomba omba wazazi pesa mara nimekwama, mara naazima.

Mimi kama mzazi nimeshuhudia walimu wa shule moja ya seminary za miaka hii maana seminari za zamani kulikuwa hakuna walimu wanaopiga mizinga . sijui wanafikiri ukipeleka mtoto shule ya mission ada iko juu basi unahela muda wote, hii ni rushwa tunailea.

shule zikifungwa mkifuata ripoti na matokeo ya mtoto mwl anasubiri kupewa vijipesa . Hivi watoto wetu mnawafundisha maadili gani kama mwl unatafuta kila mwezi kupiga mizinga wazazi wa watoto wa shule unayofundisha.

Walimu mbadilike kama mzazi atakupa ya vocha ni awe amaeamua na sio mgeuke ombaomba kama walinzi wa maegesho.
Kwenye shule za English kuna baadhi ya wazazi huwa ni hopeless sana, wewe ni mmoja wao.
 
Hivi vidada vya daycare watu wanavipelekeaga sana moto,,wakikuona kama una harufu ya visenti lazima watafute upenyo kupitia mwanao ili wakufikie,,wakianza kulia njaa wengine hawalazi damu pesa inatoka na kyupi
 
Mkuu wewe ni Jinsia gani!!!??
🤬🤬🚮🚮
 
Back
Top Bottom