Walimu naomba mjirekebishe na hili la kuomba tip

Naona walimu povu linawatoka kama lote. Shule zote nazozungumzia ni hizi za private uchwara. Moja iko kinondoni wilaya na ingine iko mkoa wa kibaha pwani. Mizinga imezidi jamani kila mtu ana majukumu na shida zake ila unapoona mwanaume mtu mzima anapiga mizinga unafikiria huko nyuma aliishiije atakuwa na marinda kweli.
Enzi zetu walimu waliheshimika sana na walikuwa viongozi hata kwenye mitaa siku hizi walimu wanavaa kata K. Wanajishushia hadhi.
 
Mtu anakaa na mtt wako mwaka mzima hata 5,000 tu ya soda kumpa ni shida? Ubahili mwingine ni useng.....kwani itakupunguzia nn as long as mapato Yao Kila mtu anawahurumia?roho mbaya tu...
 
Kwa Nini usimwambie huyo mwalimu Sasa,acha kuzingua maticha
 
Ngoja aje Kamishina wa Elimu, Mpwayugu Village atoe ufafanuzi
 
Sidhani kama kulikuwa na haja ya kujumuisha walimu wote, kwa upande wangu hii leo ndo naisikia mwalimu kuomba fedha kwa mzazi/mlezi.
 
Hali ngumu kwa walimu hata mimi ilinitokea mpaka tukawa wapenzi na huyo mwalimu
 
Mkuu mbona umehusisha jamii kwenye jambo ambako kimsingi linahusu mahusiano yako na huyo/hao walimu, kama wewe umeshindwa kumwambia huyo mwalimu mmoja hapana na kumtaka aache hiyo tabia, mbali zaidi unampa mara kwa mara hiyo unayoita rushwa basi wewe ndiye unayetakiwa kubadilika mara moja.
 
Ungewaambia trafic hii statement ingefaa sana, maana wanapiga mizinga haooooo!!!
Na bado mnatoa kwa furaha na tabasamu juu!

Walimu wale rushwa? How wakati wateja wake ni wanafunzi wasiokuwa na vipato kabisaaa!
 
Mwalimu akiomba ni kosa ila polisi, daktari, mwanasheria n.k hata kabla hawajaomba unajipendekeza kubwapa mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…