KERO Walimu Sekondari JM Kikwete ya Tunduma waache kulazimisha Wanafunzi kununua karanga

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mwalimu acha wivu mwenzako auze Karanga....sasa kama toto halina hata mia tatu bado linafeli si mzigo kwa Jamii yake.
 
Dah mwanangu miaka 5 kila ukimuuliza anakuambia askari, na habadilishi
 
Kujadili hili niupumbavu,unamtaja jina kumchafua mtu kipumbavu sana
 
Walimu itabidi waongezwe mishahara na pia hii taaluma iheshimike again, otherwise wataendelea kuchukuliwa poa kama kawaida
 
Sioni tatizo Lolote, Walimu Wana changamoto kubwa sana, graduate huyo Ujue, Hana overtime wala allowance yoyote ile wakati Serikali yake imetenga Billions kununua magari
Kwani siku hizi wanafunzi wana vitega uchumi?
 
Umefika ofisi ya mkuu wa shule kutoa malalamiko yako, vikao vya wazazi je unashiriki? umewahi kuwasilisha hiyo kero.
 
Huenda ni maelekezo kutoka kwa mwenye shule JM Kikwete, nashauri malalamiko apelekewe yeye.
 
Umaskini mbaya sana.
 
Mambo madogo hayo
 
Ni kama tu vile mchungaji anapoamua kula vya madhabauni kaka, na sidhani kma mtoto akisema hana hela huyo mwalimu atalazimisha kuingiza mikono mifukoni kwa mwanafunzi.
 
Mtoa mada unaonekana una tabia za kikuda, majungu na wivu. Na walimu wa aina yako, mara nyingi ni wale wa kupenda sana kujipendekeza kwa Mkuu wa shule, na pia kuwachongelezea walimu wengine ili mfikiriwe kwenye zile fursa za kusimamia na pia kusahihisha mitihani.

Watu wa aina yako mara nyingi huwa mnaishi kwa kutegemea mshahara kwa 100%. Ndiyo mnaoshinda shule kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 4 usiku! Huwa mnakuwa ni viherehere sana! Na ndiyo mnaosababisha kada ya ualimu idharauliwe hata na watu ambao hawajasoma!!

Ishu kama hii ilikuwa inaishia tu kwenye vikao vyenu vya staff. Wala hukuwa na sababu ya kuja kuileta humu jukwaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…