Walimu Shule ya Msingi Chanika, acheni kuwafungia darasani watoto wasiotoa mchango wa chakula

Walimu Shule ya Msingi Chanika, acheni kuwafungia darasani watoto wasiotoa mchango wa chakula

NGOSWE2

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2013
Posts
1,323
Reaction score
1,608
Katika hali isiyotarajiwa wanafunzi wameanza kupata shida mashuleni.

Iko hivi, baada ya Serikali kutoa mwongozo kwa ajili ya watoto wetu kula chakula mashuleni hali imekuwa tofauti kabisa.

Watoto wanalalamika kuwa chukula wanachopewa ni kibaya, wameenda mbali na kusema wakati mwingine kinakuwa kibichi. Kutokana na hali hiyo watoto wengi hawatoi pesa ya mchango wa chakula wanyopewa na wazazi wao na kuamua kununua kile wanachokitaka.

Sasa hili la kutotoa hela ya chukula na kuamua kununua chakula nje ya shule, wanafunzi wa shule ya Msingi CHANIKA kufungiwa darasani kwa wale wasiotoa hela ya chakula muda wa mapumziko na kuambiwa kwa lugha kali kuwa endapo watakuwa hawatoi pesa hata shule watafukuzwa.

Je, huu ndio mwongozo wa serikali uliyotolewa?
 
Lipa hio pesa acha usumbufu, bila ubandidu kama huo watu hamtatoa michango. Nawapongeza walimu, washikilie hapo hapo, mana mlikubaliana wenyewe kwenye vikao vya wazazi hio michango.

Kama hutaki wanao wale hicho chakula, toa mchango kisha uwe unawapa pesa ya kula chakula chao.
 
Hiyo serikali imepeleka chakula? Inalipa mpishi? Inanunua kuni?
Kwani maana ya kuchangia ni nini? Si ni pamoja na kununua kuni, chakula na mpishi?

Kinachozungumzwa hapa ni chakula kilichopikwa na mpishi kwa kutumia kuni kwa michango ya wanafunzi lakini ni chakula kibaya, kinachopekelekea watoto wasikipende na kuamua kwenda kununu chakula nje, kitendo ambacho kimewaudhi hao waandaji wa chakula na kuwafungia madarasani.
 
We ni mzazi? Lini watoto wakajua chakula kibichi na kilichoiva? Watoto huwa wanabugia Du

Lipa hio pesa acha usumbufu, bila ubandidu kama huo watu hamtatoa michango,
Nawapongeza walimu, washikilie hapo hapo, mana mlikubaliana wenyewe kwenye vikao vya wazazi hio michango,
Kama hutaki wanao wale hicho chakula, toa mchango kisha uwe unawapa pesa ya kula chakula chao
Pesa sio tatizo. Tatizo chakula wanachopewa hao wanaolipiwa pesa. Toa pesa pata huduma
 
Wewe chakula umekionja ukaamini kuwa ni kibaya na haijaiva??? Kulea watoto ni kazi sana na ndio maana wazazi wengi wa siku hizi hawataki kukaa na watoto nyumbani. Waache walimu wafanye kazi yao usishabikie malezi yatakayopelekea taifa la magoi goi
 
Wewe chakula umekionja ukaamini kuwa ni kibaya na haijaiva??? Kulea watoto ni kazi sana na ndio maana wazazi wengi wa siku hizi hawataki kukaa na watoto nyumbani. Waache walimu wafanye kazi yao usishabikie malezi yatakayopelekea taifa la magoi gwaka

Pesa sio tatizo. Tatizo chakula wanachopewa hao wanaolipiwa pesa. Toa

Wewe chakula umekionja ukaamini kuwa ni kibaya na haijaiva??? Kulea watoto ni kazi sana na ndio maana wazazi wengi wa siku hizi hawataki kukaa na watoto nyumbani. Waache walimu wafanye kazi yao usishabikie malezi yatakayopelekea taifa la magoi goi
Watoto hawapelekwi shule kulelewa, ondoa dhana hiyo?
 
Hayo ni ya kweli kabisa na sio shule hiyo tu, kwani Sasa imekuwa ni kama ni mradi Kwa walimu wa baadhi ya shule kulazimisha pesa na papo hapo huduma ni mbovu. Tatizo sio pesa Bali tatizo ni huduma ni mbovu na ni kinyume na makubaliano.
 
Haya tena, watoto wananyanyaswa huko, tunae mheshimiwa waziri Dkt gwajima d, natumai atakusoma na atalishughulikia hili.
 
Hayo ni ya kweli kabisa na sio shule hiyo tu, kwani Sasa imekuwa ni kama ni mradi Kwa walimu wa baadhi ya shule kulazimisha pesa na papo hapo huduma ni mbovu. Tatizo sio pesa Bali tatizo ni huduma ni mbovu na ni kinyume na makubaliano
Mkuu kuna binti yangu yupo kidato cha pili kuna baadhi ya vyakula akila tu, huyo ataumwa tumbo siku kadhaa haendi shule. Na nilitoa taarifa juu ya afya yake shuleni.

Lakini cha ajabu alikuwa anakula fimbo kwa sababu ya kutotoa hela ya chakula na kumwambia kwa nini yeye ale chakula cha tofauti na wenzake. Siku za kwanza mwanangu alikuwa anawapa hela ya bila kula chakula. Ilibidi niwafute kwa ukali ndio kumwachia mtoto anunue chakula anachoona kinamfaa kwa afya yake.
 
Back
Top Bottom