Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa haya malalamiko yako ya watoto kula chakula kibichi, si ungeyapeleka huko shule ili hiyo kasoro irekebishwe?Kwani maana ya kuchangia ni nini? Si ni pamoja na kununua kuni, chakula na mpishi?
Kinachozungumzwa hapa ni chakula kilichopikwa na mpishi kwa kutumia kuni kwa michango ya wanafunzi lakini ni chakula kibaya, kinachopekelekea watoto wasikipende na kuamua kwenda kununu chakula nje, kitendo ambacho kimewaudhi hao waandaji wa chakula na kuwafungia madarasani.
AiseeKatika hali isiyotarajiwa wanafunzi wameanza kupata shida mashuleni.
Iko hivi, baada ya Serikali kutoa mwongozo kwa ajili ya watoto wetu kula chakula mashuleni hali imekuwa tofauti kabisa.
Watoto wanalalamika kuwa chukula wanachopewa ni kibaya, wameenda mbali na kusema wakati mwingine kinakuwa kibichi. Kutokana na hali hiyo watoto wengi hawatoi pesa ya mchango wa chakula wanyopewa na wazazi wao na kuamua kununua kile wanachokitaka.
Sasa hili la kutotoa hela ya chukula na kuamua kununua chakula nje ya shule, wanafunzi wa shule ya Msingi CHANIKA kufungiwa darasani kwa wale wasiotoa hela ya chakula muda wa mapumziko na kuambiwa kwa lugha kali kuwa endapo watakuwa hawatoi pesa hata shule watafukuzwa.
Je, huu ndio mwongozo wa serikali uliyotolewa?
Yani mkuu wazazi wa kipindi hiki wanamalezi mabovu kweli kwel sisi tumesoma boarding huko tumekula vibichi matumbo yakauma na tumepona tuko hapa leoNinachojua shule hakuna chakula kizuri,kitamu,kibichi wala kilichoiva. Au kwasababu hyo shule ipo daslam?
Na mnashabikia kabisa mtoto anasema chakula kibaya! smhDuh Pole! Ninako kajukuu kangu kana miaka miwili chakula kikiwa kibaya kanasema, hiki ni kibaya. Sembuse watoto wa shule ya msingi!
Kwakuwa hela zinaokotwa ....Lipa hio pesa acha usumbufu, bila ubandidu kama huo watu hamtatoa michango. Nawapongeza walimu, washikilie hapo hapo, mana mlikubaliana wenyewe kwenye vikao vya wazazi hio michango.
Kama hutaki wanao wale hicho chakula, toa mchango kisha uwe unawapa pesa ya kula chakula chao.
[emoji23][emoji23][emoji1787][emoji38][emoji38]Toa mchango bwana acha kulialia