Walimu wa Hisabati, hii inaweza kutusaidia kufaulisha Wanafunzi na kulipenda somo hili

Walimu wa Hisabati, hii inaweza kutusaidia kufaulisha Wanafunzi na kulipenda somo hili

Kijana ushe2

Senior Member
Joined
Apr 6, 2017
Posts
179
Reaction score
127
Habarini za humu JF Elimu,

Leo nimekuja kutoa nami mawazo na mitazamo ni namna gani tunaweza kuwasaidia hawa watoto katika hili somo rahisi kabisa!

MAMBO YA MSINGI KWA MWANAFUNZI NA KWA MWALIMU
1. Lugha adhimu ya kiingereza iwe mikononi mwa wanafunzi kwa vyovyote vile hasahasa grammatical and structure of language (even introduction).

2. Mazoezi ya mara kwa mara kwa mwanafunzi na ikiwezekana wanafunzi wasimamiwe waache uzembe wa kushindwa kufanya maswali kila mara wakiwa nyumbani au shuleni.

3. Upendo na utii kwa mwalimu hufanya mwanafunzi apende somo hili na hapo sisi walimu wa hisabati tukubali challenge na tukubali kujirudi na kuwasaidia zaidi watoto na kufanya maswali mengi hasw na kuwapatia moyo wa kupambana.

4. Mitihani na majaribio ya mara kwa mara kutolewa na walimu, hii itasaidia mwanafunzi kuwa makini na kuwa na mwanga zaidi wa maswali yanavyotoka na mitego gani hutokea kwenye maswali!!!

5. Walimu wa hisabati wapewe zawadi zozote na serikali ama halmashauri pale wanapofanya vyema katika somo hili kwani walimu wanaweza wakawa wanatumia mpk muda wa ziada kabisa kwa ajili ya wanafunzi.

MAMBO YANAYOSABABISHA SOMO HILI WANAFUNZI KUFELI
1. Uwezo binafsi wa mwalimu unakuwa wa chini(self management in teaching maths) hii inafikirisha saana lakini ukweli ni kuwa walimu huwa hatutumii njia mbadala za kufundisha na wengi wetu tunaamini wanafunzi wanajua vitu vichache saana na wale ambao hawawezi huanza kutengwa na mwalimu kitu ambacho si kizuri kabisa.

2. Upungufu wa wataalamu wa hisabati (walimu wachache wa somo husika) hii inafanya wanafunzi wasisome hili somo. Hivyo kama serikali inataka kulifanya somo hili lisiwe na ufaulu hafifu inabidi waajiriwe walimu wa somo hili kufuatana na mahitaji ya shule kwa Tanzania nzima nje ya hapo tutakuwa tunalalamika kila kukicha.

3. Uwezo wa wanafunzi toka shule ya msingi ni mbovu mno. Serikali iajiri walimu haswa kwa shule za msingi ambao watakuwa na uwezo wa kufanya somo liwe rahisi zaidi na watoto waelewe msingi use imara zaidi.

Kwa leo naishi hapa nataka maswali na maoni zaidi kuhusu hili somo letu pendwa.
 
Si tuliambiwa Math is not for all.
 
Back
Top Bottom