Walimu wa Shule ya Sekondari Ilala, kwanini mnauza notes kwa wanafunzi?

Kwa wanafunzi wetu huu mfumo hauwafai maana tutazalisha vilaza waliofaulu
Sasa watunga sera wako ndiyo wamepitisha hiyo sera. Tena ni watu wenye Ma PhD yao! Na mbaya zaidi watoto wao wanasoma kwenye shule binafsi kama FEZA zenye kila kitu!

Halafu watoto wa wanyonge ndiyo hawa ambao baadhi ya walimu wanajaribu kujiongeza ili kuwasaidia, wazazi nao kwa uelewa wao mdogo! wanakuja juu!
 
Kimsingi mwalimu anatakiwa atoe option! Mwenye uwezo wa kununua, anunue ili kuokoa muda wa kuandika. Asiye na uwezo aandike.

Iwapo atalazimisha wote kununua! Tena kwa adhabu au vitisho kwa wale ambao hawana hiyo hela, hapo inakuwa ni tatizo. Busara ndiyo kila kitu kati ya mwalimu, mwanafunzi na mzazi.
 
Ubao ni wa kufundishia ni kama rough paper tu sio wa kuandikia notes..mwalimu una dk 45 mpaka 90 tu z kufundisha darasani muda wa kuaaandikia notes ukowapi...hiyo 200 inakushinda nini
 
Na tatizo ka dunia ya sasa reward ni monetary..., zamani mwalimu akiona mtoto alikuja kilaza akamsaidia hata kuondoka na wastani wa average yaani anajisikia Job well Done..., kwahio unakuta anatumia kila mbinu ili kumvuta mwanafunzi na kumfanya apende kusoma...

Sio kutimiza wajibu tu..., ila ndio dunia ya sasa mtu hapendi kazi yake ni basi tu huko ndio mkono unakwenda kinywani

Ingawa binafsi naelewa kujitafutia materials mwenyewe unaelewa zaidi kuliko kupewa summaries (ila ndio hivyo wote hatupo sawa) yaani unakwenda an extra mile....,
 
[emoji444][emoji444]Ukiwaa unaona elimu ni ghali basi jaribu Ujingaa eliii chinyamaa msimamishee msimamisheee aoneee[emoji444][emoji444][emoji444]Banza Stone RIP
 
Yaan unalalamika kununua notes za 200 dah?? Wakati ilitakiwa walimu mjichangishe walau 10,000 kwa mwa mwez muwape walimu motisha wawafaulishieni watoto wenu waje kuwasaidia nyie wenyewe!! Mwache asisom,akauze mitumba karume mbona siyp mbali na hapo
 
Kama wote wanaomsakama mwalimu ni wazazi basi taifa lilipata kuwa na vijana wa hovyo sana huko miaka ya zamani
 
Pia Kuna wazazi wengine ni wahovyo mno hasa Kama huyu amekazania kuwa mwanae aandikiwe notes ubaoni Kama zamani [emoji44][emoji44][emoji44] ewe mzazi Kila zamanankitabu chake tangu wewe unasoma Hadi Leo mambo yanaenda mbio Sana,
Kama hutaki mwanao auziwe hizo notes jitahidi umnunulie mwanao vitabu vya masomo husika ilu kumwandaa mwanao kufauru hate bila ya kupewa hizo notes, Nchi zilizo endelea huo mfumo was notes haupo kabisa kwakuwa k
Mtoto anaelekezwa tu kwa ufupi kuhusu mada husika ili kupata maelezo zaidi akajisomee kitabu na Kama Hana mwalimu anamsaidia kwa kumoatia hizo notes Kama mbadala wa notes, Nina mengi ya kukueleza lakin kwa leo niishie hapo Cha zaidi mshukuru huyo mwalimu analengo la kumsaidia mwanao pamoja umasikini uliopo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We we mzazi hiyo hela Ni ndogo Sana,toa,nimefanikiwa kuviona vitabu vya bure vinatolewa na TIE(Tanzania institute of education) material yake yako shallow Sana,yaani masomo mengi tu,Sasa mwalimu akitaka kwenda zaidi ya hapo inabidi azalishe vimatini vya ziada ya pale ,vile anaenda kuvizalisha stationary,kwa gharama fulani ,Sasa ametumia gharama anatoaje bure, Hilo la Kwanza,la pili katika kusoma Kuna vitabu vya kiada(vya kufundisha vilivyopendekezwa na TIE) na vitabu vya ziada alivyosoma mwalimu na kuvitengenezea matini,ukweli labda pigania shule ziwe na stationary ili watoe materials hizo bure,hapo bure itawezekana
 
Na nyie zitengenezeni muwagawie watoto wenu. Notes sio kazi ya mwalimu. Kazi ya mwalimu kufundisha. Mwanafunzi amsikilize mwalimu na ajiandikie notes. Wale wavivu hawana namna wajinunulie tu!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna ELIMU Bure. Nawashauri walimu wapandishe Bei kwani vita ya Ukraine bado ipo na mafuta yanapanda bei
 
Unachojua ni kunyandua tu na mimba itokee, kulea hujui. Yaani mwanaume unaona shida kitoa 200?!! Mxyuuu na mwezi ujao naanza kuuza 500
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…