Walimu wa Tanzania na passive resistance

Walimu wa Tanzania na passive resistance

Hali ni mbaya sana,Kuna mtoto unamfundisha unaamini necta hatoboi,cha kushangaza matokeo yakija ana division 1,usahishaji wa mitihani nao Kuna changamoto,kiifupi elimu imeingiliwa,tusifurahie matokeo kwani hayaakisi uwezo wa mtoto,kiufupi Gori limetanuliwa Kila mtu afunge
 
Hili bomu lita kuja kulipuka in some few years to come.
Lilishalipuka kitambo mbona? Ndo maana watu wanaambulia kuwa na vyetu tu lakini maarifa hakuna! Mtu ana degree au masters au PhD lakini hajielewi kila siku kutembeza bahasha ya kusaka ajira
 
Hizo ni fijra zako potofu tu.

Usifanye wakapewa "passive dose".

Umesahau mgomo wa dakatari ulimalizwa vipi?
Hebu fanya urekebishe basi hiki ulichokiandika hapa. Isije ikawa na wewe kumbe ulienda shule kusomea ujinga. ....fijira! ...dakatari!! Ndiyo utopolo gani huu!! 😁
 
Na huo ndio mgomo mbaya kushinda migomo yote!
Tunaoumia ni sisi wenye watoto.
 
Tuition zilipigwa Marufuku na serikali, siyo kwamba walimu hawataki kufundisha muda wa ziada.

Kama madaktari wanaenda private baada ya kutoka hospitali za serikali unadhani walimu wasingependa kufundisha tuition baada ya muda wa kazi za serikali au siku za mapumziko kama jumamosi na jumapili?

Wanapenda lakini katazo la serikali yao ambaye ndiye muajiri wao.
ni walimu wachache sana waajiriwa wenye Nia ya kufundisha tuition kwa Karne hii,wengi wamejikita kwenye biashara vyao tu sio kama zamani
 
Hali ni mbaya sana,Kuna mtoto unamfundisha unaamini necta hatoboi,cha kushangaza matokeo yakija ana division 1,usahishaji wa mitihani nao Kuna changamoto,kiifupi elimu imeingiliwa,tusifurahie matokeo kwani hayaakisi uwezo wa mtoto,kiufupi Gori limetanuliwa Kila mtu afunge
[emoji1666][emoji1666][emoji1666][emoji1666][emoji1666]
 
Bro uliosema ni si sahihi ila kuna sababu nyingi saana inayofanya sasa hivi mambo yawe tofauti hapa ntaandika kama mwalimu wa kijijini ndani ndani huko:
  1. Mazingira magumu ya kazi kwa walimu siku hizi ya kazi (nyumba mbovu yaani nyumba inakuuliza nikuangukie lini mwalimu) kwani kuna baadhi ya vijiji hakuna hata nyumba za kupanga mfano ktk shule yangu mwlm mkuu anakaa na walimu wanne. Nyumba moja.
  2. Bro. Wazazi wa sasa wana roho mbaya sijawahi kuona mzee walimu wakipelekewa kuni na wanafunzi jau, akifatiwa maji jau, wakimsaidia shuguli ya shamba jau, mwalimu akiuza hata kashata jau hivyo mwalimu anaona bora atafute mishe ya kufanya ili maisha yaende.
  3. Twende pamoja hapa. Kipindi tunasoma sisi wa 1985s mwalimu alikuwa akija kwenu lazima ukahadithie shuleni na akitoka hapo atazawadiwa mayai, maziwa, karanga n.k lakini wazazi wa sasa wana roho mbaya saana sijui n umaskini au lah.
  4. Serikali ndio imekuja kuharibu kabisa kwenye suala la nidhamu. Kwanini nasema hivi ni kwasababu serikali ilitoa waraka wa viboko mashuleni mtoto kumuadhibu mwisho fimbo mbili na lazima achapwe na mwl mkuu au mwl mkuu ndio akuruhusu na kama n wa kike ataadhibiwa na wakike sasa em angalia huo mlolongo wa kutoa adhabu si bora uachane nae akavute bangi huko.
  5. Wazazi sasa hivi wamezidi kulalamika saana mwalimu anakuja na mpango kazi ya kuwafanyisha watoto mazoezi na majaribio la kila wiki lakin shule haiwezi Kugharamikia anawashirikisha wazazi kuchangia hata mia tano lakini wazazi watakapo andamana hapo mmmh. Kuna shule moja wazazi waliwahi kuuliza kuwa kwani hata watoto wao wakifeli walimu itawauma nini?.
  6. Serikali iboreshe maslahi. Narudia tena serikali iboreshe maslahi
 
Tuition zilipigwa Marufuku na serikali, siyo kwamba walimu hawataki kufundisha muda wa ziada.

Kama madaktari wanaenda private baada ya kutoka hospitali za serikali unadhani walimu wasingependa kufundisha tuition baada ya muda wa kazi za serikali au siku za mapumziko kama jumamosi na jumapili?

Wanapenda lakini katazo la serikali yao ambaye ndiye muajiri wao.
Unaishi wapi ndugu, sasa hivi walimu wame-advance, tuition zinafundishiwa shuleni na walimu husika, Mimi nina mtoto anasoma Nyampulukano secondary Sengerema, kidato cha pili, darasani wako 600+, wametakiwa wote kusoma wiki 3 kwa malipo ya 5,000/= hapo hujaweka wa kidato cha 4 ambao ni 400+, Nina mtoto darasa la 5, hapa hapa Sengerema hizo wiki 3 nimelipa elfu 10,000/=, Sengerema karibu shule zote mwendo ni huo, wengine wanashughulika na madarasa ya mitihani wengine hadi chekechea, hivyo ni namna ya kuoperate hizo tuition ndiyo kumebadilika.
 
Hali ni mbaya sana,Kuna mtoto unamfundisha unaamini necta hatoboi,cha kushangaza matokeo yakija ana division 1,usahishaji wa mitihani nao Kuna changamoto,kiifupi elimu imeingiliwa,tusifurahie matokeo kwani hayaakisi uwezo wa mtoto,kiufupi Gori limetanuliwa Kila mtu afunge
Matokeo yawe mabaya wakati tunapokea pesa za wafadhili! Thubutu.
 
Hali ni mbaya sana,Kuna mtoto unamfundisha unaamini necta hatoboi,cha kushangaza matokeo yakija ana division 1,usahishaji wa mitihani nao Kuna changamoto,kiifupi elimu imeingiliwa,tusifurahie matokeo kwani hayaakisi uwezo wa mtoto,kiufupi Gori limetanuliwa Kila mtu afunge
CCM wanapika takwimu
 
Back
Top Bottom