Kwani walimu ndo Tume ya uchaguzi??
Wanasimamia Chaguzi zoooote km wewe sio Mwl basi huna kigezo muhimu cha kusimamia uchaguzi kuanzia Serikali za Mitaa mpaka Uchaguzi Mkuu wasimamizi ni Walimu, wao ndio wanapewa kipaombele sababu hawana marupurupu kwenye kazi yao kwa hio linakua km dili sasa upewe dili halafu ufanye kinyume na aliekupa dili wewe utakua una akili?
Baada ya hapo anapandishwa daraja au anapewa uafisa elimu kata au mkoa ndio malipo hayo ya Wanasiasa, uelewe hapa wanaopewa vyeo na kupanda madaraja sio wasimamizi wa kawaida nazungumzia Wakuu wa Kituo cha Uchaguzi, baada ya hapo anaachwa hapo anakula msoto miaka mitano mbele ndio anakumbukwa kwenye uchaguzi mwingine anaenda kusimamia akipewa 500,000 Mwl hio ni pesa nyingi kwake yupo tayari kuingiza sanduku lenye kura zilizokwishapigwa tayari kwenye kituo cha wapiga kura kisa 500,000 huyo ni Mwl
Akipewa 500,000 yupo tayari kutangaza matokeo tofauti yasiyo sahihi na kura zilivyopigwa huyo ni Mwl usishangae 500,000 hio 500,000 kwa Mwl ni pesa nyingi asikwambie mtu na usiulize kwanini ila tambua Walimu wengi wanaishi na Madeni ya Mikopo yanayotakiwa kulipwa mpaka siku wanastaafu Penseni yao itaendelea kukatwa na Bank sababu ya Madeni mfululizo yaliyolimbikizana huko Bank, kwenye Maduka, Vibanda vya Mobile Money, nk kote wanadaiwa ni madeni mfululizo, sababu hawana hela inabidi wakope Walimu wengi ni mitaji ya Mabank na wafanyabiashara wa Maduka sababu Walimu wanakopa sana, kwa hio ni rahisi kununulika na Wanasiasa kuwatumia vibaya baada ya kuwatumia wanawabwaga huko
Na kingine usichokijua Walimu wote wanaofanya kazi Serikalini hapa nataka nieleweke ninaposema wote namaanisha wote waliopo Serikalini ni Wanachama wa Chama A na wale wasiosimamia uchaguzi ukifika uchaguzi ni lazima wapige kura na ni lazima wakipigie Chama A na Mgombea wake hio sio hiari ni lazima ni kuna vita kali huko za kuchongeana ukionekana wewe una viashiria vya kiupinzani pinzani unachongewa kwa alie juu yaan haukubariani na Chama A unaitwa unapewa onyo au unatengenezewa zengwe la kufutwa kazi
Walimu wote wa Serikali wana uniform za Chama A uwe unapenda uwe haupendi Chama A kwanza ndio masuala yako mengine ya ualimu yanafuata na kukiwa na ziara ya kiongozi yoyote wa Chama A au anaehusiana na Chama A walimu lazima wawe mstari wa Mbele kwenye mahudhurio ni lazima kuhudhuria kwenye hio ziara ya kiongozi sio hiari ni lazima na kumsikiliza huyo kiongozi iwe unataka au hautaki yaan sehemu yoyote ukisikia kiongozi fulani kaja au amefika Mkoa fulani anazungumza na Wananchi mfano kiongozi wa Mbio za Mwenge amefika basi 90% ya watu waliohudhuria pale na unaowaona pale kwenye mkutano ni Walimu ukiondoa watu wengine (hii ilinishangaza) na kwenye shughuli za Mwenge Walimu wanatakiwa kulala palepale na ule Mwenge mpaka utakapoondoka hakuna kwenda kulala nyumbani na usichojua ni kwamba wanapitisha mpaka attendance kabla na baada John Nipo James Nipo Jasmin Nipo km haupo utaeleza kwanini haukuwepo kiongozi alipokuja ulikua wapi hujatoa taarifa utachongewa upoteze kazi na kazi unaitaka hao ndio Walimu
Walimu waliofanya kazi Muda mrefu Serikalini ndio wana maendeleo walau na angalau uwezo wa kukopa Bank mpaka Million 30,40,50,60,70 au 80 hio priority wanayo ila sio maendeleo yale sababu ya kuishi na madeni pesa haitoshi, kwa hio Wanasiasa wanatumia mwanya huo huo kuwatumia kisha kuwatupa pembeni huku wao wakipiga hela nyingi huko Bungeni