Walimu wana wakati mgumu! Darasa limejaa wanafunzi zaidi ya mia moja hana hata pa kukanyaga!

Walimu wana wakati mgumu! Darasa limejaa wanafunzi zaidi ya mia moja hana hata pa kukanyaga!

Lwezera shule ya msingi, naijua vizuri sana hii shule. Pale hakuna uhaba wa vyumba vya madarasa kwa kiwango hiki mpaka wanafunzi wajae hivi.
Huenda huyu mwalimu aliunganisha mikondo yote akawaweka kwenye darasa moja ili ionekane kuna shida kubwa kiasi hiki.
mwalimu ndo atajua sasa madhara ya mitandao,hii imekula kwake
 
Katika pitapita zangu nimekutana na hii video ikionesha wanafunzi walivyorundikana kwenye chumba cha darasa kama ng'ombe tena wakiwa wamekaa chini, na bado tukiendelea kupiga makofi kuhusu ununuaji wa madege ya dreamliner. Kama Taifa tunapaswa kupaza sauti zetu kama wananchi wa Taifa Tanzania maana haya yanatokea hapa hapa nchini.


Pamoja na kuwa sina nia ya kupinga kuwa bado kuna changamoto za Elimu nchini ILA
mtu mwenye taaluma ya Ualimu ANAONA WAZIWAZI KUWA VIDEO HUSIKA IMETENGENEZWA/IMEIGIZWA na aliye jifanya ni Mwalimu, anaonekana kabisa yupo kazini (muigizaji) wala sio mwalimu wa shule husika na huku wanafunzi wakijitahidi wasimcheke. Inaonekana kakusanya wanafunzi wa mikondo kadhaa ili kufikisha ujumbe wake alio kusudia.

Ni vizuri Watanzania tuwe WAZALENDO kama mataifa mengine yanavyo penda Nchi zao; Laiti watanzania wangefanikiwa kwenda au walau kukutana na wazalendo wa Nchi ya America au Pengine Nchi za Ulaya; hutawahi kuwasikia wakiongea lolote baya kuhusu Nchi zao...sio ndio kujivua nguo sijui ndio kufanya tuonewe huruma/tusaidiwe???
Hii inamaanisha tuwe na utaratibu wa kuonesha tatizo kiuhalisia kwa nia ya kulifanya lifahamike na litafutiwe ufumbuzi...

Kwa baadhi ya watanzania hasa Vijana nahisi kuna mahali tunakosea; kwani tunatumia muda mwingi kujivua nguo badala ya kujivunia vitu vyetu. Yaani mtu akiwa na wageni anatumia muda mwingi kuongea madhaifu hadi wanamshangaa kwamba, wao wameona Nchi ni nzuri ndio maana waka amua kuitembelea yeye haoni chochote?

Mf:
Hata mtu akisema mbuga ya Serengeti ni nzuri sana , utasikia inafikia Okavango delta ya Botswana???
Mtu akisema Mbwana Samata anafanya Vizuri sana kwenye michezo; utasikia Amebebwa???
Ukiambiwa Timu ya Simba inafanya vizuri, utasikia wamekwenda kwa mganga??
Ukisema chuo kikuu flani kinajitahidi; utasikia kile hakuna kitu...wakati mtu mwenyewe anapas za kuunga unga?
Hapo Hujamsifia Rais au baadhi ya Mawaziri ambao ni outstanding??
nk
Naona kabisa kuna mahali tunakosea?>>>>>>
NI LAZIMA TUWE WAZALENDO NA KUPENDA VITU VYETU NDIO WENGINE WAVIPENDE...
 
Kalamu1,
Utawasikiaje wakati hatuwapi support? Wao kila siku mahakamani, mikutano imezuiwa ila ccm ruksa, bunge limekuwa gizani utaskia wapi? Vyombo vya habari wanatishwa kuandika au kuonyesha kazi yao kuenyesha ikulu live tu.
Sikubaliani na hili mkuu wangu 'Return', na mawazo yangu juu ya hili yako wazi humu JF.

Kama wapinzani kazi yao ni siasa, ina maana miaka yote minne wamekuwa hawafanyi kazi?

Kutofanya kazi kwao ndio sababu mojawapo ya huyo anayewavuruga aendelee kuwakalia vichwani. Ndio, wamewekwa jela , n.k., lakini hiyo haitoshi kuwa mwisho wao wa kufanya kazi, huku wakiendelea kupata marupurupu yao kama kawaida.

Nisikupotezee muda mwingi. Ukweli ni kwamba bado hatuna upinzani wa kweli; tunao upinzani wa maslahi kwa sasa hivi.
 
Acheni umbumbumbu na nyie jamani. Dreamliner ziko hapa kukuza uchumi na siyo starehe. Jaribu kufikiria kama zisingekuwepo sasa hivi ingekuwaje? Maana ndugu zangu Precision weshatepeta na matapeli wetu Fastjet weshakata pumzi kitambo. Kwa videge viwili sijui vitatu vya precision nauli ingeshafika milioni mbili kwenda tu hapa KIA. ATC ni lazima iwepo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Dreamliner zinakuza uchumi! Hatufugi kuku unaodhani tutauza mayai na nyama nje ya nchi. Ethiopia wanaujuzi wa biashara ya usafiri wa anga miaka mingi sana, wao hata wakati ule wa vurugu nchini mwao shirika halikutetereka na wanazo ndege nyingi sana lakini hazijaweza kukuza uchumi wa nchi yao. Tueleze ni mabadiliko yapi zimeleta nchini kiuchumi kuliko kisiasa. Tangu zije zimeleta watalii wangapi nchini! Watalii huletwa na ndege zao siyo kama Uber unaipigia simu inakuja kukubeba. China tulikuwa tukiicheka miaka ya sabini lakini waliwekeza kwenye elimu kwa mfumo wao wa fastafasta na sasa China si ile ya fikra za mwenyekiti. Tatizo letu ni ujenzi wa nchi kutokuwa shirikishi yaani CCM inaamini itaijenga nchi kwa kutumia wanaccm tu ili sifa na pongezi ziwe zao! Hii ni ndoto.
Tunahitaji tuwekeze kwanza kwenye elimu kwa mtindo wa fastafasta siyo huu wa Uingereza ambao mwanafunzi anasoma miaka kumi na Tisa mpaka ishirini mwisho wa siku hapati ajira anaishia kufanya kazi za kuungaunga ambazo hakusomea! Hebu nirudi kwenye elimu ya mwingereza, enzi zile shule za msingi zilimwandaa mwanafunzi kwenye masomo ya kujitegemea kilimo, ufundi na domestiki kwa wasichana, viongozi wetu wakasema eti wanaandaliwa kumtumikia mkoloni! Na sisi kwa ujinga tukaitikia licha ya kuwaona waliomaliza la nane wakifaidika na elimu hiyo! Useremala na uashi vilifundishwa kwenye shule za kati yaani Middle School na madeski na madarasa yangeweza kujengwa na mwanafunzi wakishirikiana na mafundi wenye uzoefu.
Tujifunze kutoshabikia na kutetea kila jambo ilimradi limeletwa na viongozi wa chama eti changu.
Mwisho kinachotokea sasa ni uzembe wa viongozi kutojua idadi ya mwanafunzi wanaoanza mwaka huu wangapi kutokana na kutokuwa na sensa ya watu, pia kutumia idadi iliyoanza leo baada ya miaka saba wataingia la tisa hivyo tujiandae mwaka mmoja kabla ya miaka saba. Mawaziri wamejikita sana kwenye safari za akina Magellan wakidhani ndiyo utendaji uliotukuka.
 
Ume

umefanya utafiti na kuuliza vyanzo vya hiyo clip na kujua nini kilitokea ktk hiyo clip mpaka wanafunzi hao wakawa humo ndani?
Critical thinking is evasive to you i am afraid...
Unaweza kuwa umesoma shule za kisasa.Lakin sisi tuliosoma shule hizo tunatambua kabisa kuwa hiyo ni kawaida.Kwa mfano hapo ukicheki hilo darasa ni kwamba kwanza mwalimu ameunganisha madarasa 2.Hii inafanyika ili kukimbizana na mtaala kwa sababu ukisema ufundishe maana ya mazingira la 5 A,B, na C basi mpaka mwezi wa 8 utakuwa topic na 4 kati ya topic 12.kwa hiyo hapo ni kwamba kuna upungufu wa walimu na pia kuna upungufu wa vyumba vya madarasa.kama unabisha jaribu kupita hata shule 2 au 3 za mjini kwenu utaona hiyo kesi ikitokea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wajuba hapo mbele kabisa wao hawana taim, wanaangalia nyuma ya darasa
 
Katika pitapita zangu nimekutana na hii video ikionesha wanafunzi walivyorundikana kwenye chumba cha darasa kama ng'ombe tena wakiwa wamekaa chini, na bado tukiendelea kupiga makofi kuhusu ununuaji wa madege ya dreamliner. Kama Taifa tunapaswa kupaza sauti zetu kama wananchi wa Taifa Tanzania maana haya yanatokea hapa hapa nchini.

Kama taifa, bado hatujajua kipi kitangulie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo lipo kwa wawakilishi wetu wa majimbo maana wao wenyewe ndo wahusika wakuu kwa hii kadhia,wanatakiwa kumdhibiti huyo anayejichotea hela yetu na kununua vitu visivyoakisi na kugusa shida za wananchi. Huku mikoani kuna shida jamani watoto wanapata shida hasa sehemu ya kukaa!!!!wakati huohuo vitabu havipo mashuleni. Tuna safari ndefu sana kama taifa
Halafu anawashangaa askari kujipangia bajeti yao bila kupitishwa na bunge wakati wamemwiga yeye mwenyewe kujichotea atakavyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika pitapita zangu nimekutana na hii video ikionesha wanafunzi walivyorundikana kwenye chumba cha darasa kama ng'ombe tena wakiwa wamekaa chini, na bado tukiendelea kupiga makofi kuhusu ununuaji wa madege ya dreamliner. Kama Taifa tunapaswa kupaza sauti zetu kama wananchi wa Taifa Tanzania maana haya yanatokea hapa hapa nchini.

Kwanini usitaje jina la shule na mkoa ili wasaidiwe?Labda hiyo picha ni ya Msumbiji au uzushi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom