Hili mbona kama ni igizo? Mpiga picha kakaa kwenye angle ambayo kachukua video kwa utulivu huku na huyo "mwalimu" akifundisha kwa mbwembwe kabisa akiwa anajua lazima aweke pozi ili kuendana na script
Huyo mwalimu gani anaingia darasani kwake anawaambia wanafunzi wake wa kila siku "mpoo?, Darasa la ngapi?" Na wao wanajibu "darasa la nne".
Sijui wala sipingi dhamira ya waliocheza sinema hii lakini angalau wangesema kweli tu kwamba kuna maofisa wa NGO au waandishi wa habari wametembelea shule fulani wakaruhusiwa kuingia darasa lililojaa wanafunzi na kufundisha huku wakipigana picha na kuchukua picha za video