A
Anonymous
Guest
Walimu wapya Wilaya ya Bukombe fedha za kujikimu tulitakiwa kulipwa kiasi cha takribani shilingi 950,000 lakini hadi sasa tumelipwa shilingi 280,000 tu. Hatujapewa maelezo ya wazi kuhusu sababu ya kupunguzwa au kucheleweshwa kwa sehemu iliyobaki ya fedha hizo.
Kinachotushangaza zaidi ni kwamba watumishi wapya wa idara ya afya tayari wameshalipwa fedha zao zote, jambo linalotufanya tujiulize changamoto iliyopo ni nini katika Idara ya Elimu.
Uongozi wa Halmashauri ya Bukombe utupe ufafanuzi na kuhakikisha tunalipwa fedha zetu zote kwa wakati.