A
Hizo 950,000/= mmetumia kigezo gani?Walimu wapya Wilaya ya Bukombe fedha za kujikimu tulitakiwa kulipwa kiasi cha takribani shilingi 950,000 lakini hadi sasa tumelipwa shilingi 280,000 tu. Hatujapewa maelezo ya wazi kuhusu sababu ya kupunguzwa au kucheleweshwa kwa sehemu iliyobaki ya fedha hizo.
Kinachotushangaza zaidi ni kwamba watumishi wapya wa idara ya afya tayari wameshalipwa fedha zao zote, jambo linalotufanya tujiulize changamoto iliyopo ni nini katika Idara ya Elimu.
Uongozi wa Halmashauri ya Bukombe utupe ufafanuzi na kuhakikisha tunalipwa fedha zetu zote kwa wakati.
Why? Mbaya sana hiiPoleni lakini hapo angalia muda walioajiriwa hao wa idara ya afya na ulioajiriwa wewe.
Kama wote mmeajiriwa sawa basi inawezekana idara ya afya wamelipa waajiriwa wao kwa OC. Na kama wamelipwa kweli basi idara ya afya ulipo inajitahidi.
Halmashauri nyingi ingawa wana OC hua inachukua muda mpaka miezi 9 kuwalipa.
MEO na VEO hupitisha mpaka miaka minne hawajalipwa pesa ya kujikimu
Boss unauliza why kwenye maswala ya tamisemi?Why? Mbaya sana hii
Ni maksudi ama?Boss unauliza why kwenye maswala ya tamisemi?