Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Ushauri umetolewa kwa Walimu nchini kuondokana na mikopo ya kausha damu na badala yake waitumie Benki ya Biashara ya Mwalimu (MCB) kwa ajili ya kuikuza na kujinufaisha wao wenyewe.
Wito huo umetolewa na Wanahisa wa MCB wakati wa mkutano wa saba wa wanahisa mwaka 2023 uliofanyika Jijini Dodoma ukikutanisha wanahisa ambao ni walimu wastaafu na waliopo kazini.
Mwanahisa Mwalimu Romana Kimambo kutoka Wilaya ya Kisarawe, amesema benki hiyo ni kitega uchumi cha walimu wote hapa nchini kwa kuwa wameshiriki kuwekeza mtaji wa benki yao.
Mwalimu Eliud Ole Mtambala wa Shule ya Msingi Chamwino, Manispaa ya Dodoma amesema haoni sababu ya Walimu kutumia benki nyingine wakati taasisi yao ipo na inaweza kuwavusha huku ikiwaheshimisha.
Mwalimu Mtambala amesema "Nina wahurumia walimu wenzangu, natoa rai wajitoe huko walikokamatika, waje MCB iwape matumaini na uhakika wa kiuchumi."
Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa MCB, Francis Ramadhani alisema thamani ya benki hiyo imekuwa kutoka sh. bilioni 30 hadi Sh. bilioni 83.
“Nataka kuwahakikishia wanahisa wote, mageuzi makubwa yanayoendelea kufanywa ndani ya benki yetu, ni ya msingi na yamesaidia kuiinua MCB hatua kwa hatua hadi mwaka 2022.
“Tumefikisha miaka saba mwaka 2022 katika utoaji wa huduma tangu benki ianzishwe, na katika kipindi hicho benki imeweza kukuza mali na thamani yake kwa zaidi ya mara mbili.
"Ninawashauri walimu waje wapitishe mishahara yao yaani wakiitumia vema benki hii nawahakikishia itakuea kubwa sana," alisema ndugu Francis.
Mwenyekiti huyo ameeleza MCB imeongeza mapato kutoka Sh. bilioni 2.8 hadi Sh. bilioni 7.2 bilioni wakati kitabu cha mikopo kikifikia sh. bilioni 64 kutoka Sh. bilioni 16 huku amana za wateja zikifika Sh. bilioni 60 kutoka Sh. bilioni 11 za awali.
Pia soma:
- Walimu watakiwa kuacha kukopa Mikopo ‘Kausha damu’

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Mwalimu Commercial (MCB), Francis Ramadhani.

Mmoja wa wanahisa wa MCB akizungumza jambo kwenye mkutano huo.
Alisema kwa miaka saba ya uhai wa MCB imefanikiwa kufungua ofisi nane za kanda katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Arusha, Kigoma, Rukwa na Mtwara ili kuwafikia wadau kwa urahisi na mawakala wa benki hiyo kila wilaya.