Ulitaka watumie G.P.A ungeweza kama maswali 25 yanakushinda…hata hivo maswali 25 ni mwanzo tu kuna oral ambayo wanafanya assessment ya uwezo wa mwalimu ku-deliver shida iko wapiMwalimu bora utampata kwa maswali ya kuchagua 25 si ndio
anayeliaMbona sisi kada nyingine tunafanya interview tatu ( written, practical, oral) na hatulii wala hatuundi chama....
Acheni kulia lia someni
Sikuzote serikali ilikua inatoa ajira kiduchu tamisemi mpaka kuna kipindi walitoa 6000 na hakuna aliyeita media , leo ajira zaidi ya elf kumi kelele nyingi … swala hapo ni USAILIMkuu hivi umewasilikiza hao vijana mwanzo mwisho ukawaelewa kweli?
Mama nae kaingia kwenye mfumoYule mrombo ni very arrogant, ana egoism, anajiona anajua kila kitu, ameharibu elimu kuanzia mitaala. Ananyanyasa walimu anavyojisika ndio maana analalamikia protokali ya ikulu. Halafu kwanini watu wasiseme huu ni Rais wa kuambiwa.
Kwaiyo unataka watu waendelee kufumbia macho tatizo liendelee kuwa kubwa kwa kigezo cha kuwa tatizo halijaanza leo bali limeanza zamani. Ndicho unachomaanisha mkuu?Kwani serikali kutoa ajira kiduchu wameanza leo mbona kipindi hiki ndio maneno yamekua mengi
Ufisadi tupuHaka kautaratibu kainterview kuna watu kamewafaidisha sana wanataman kila mwaka kawepo watu wanakadiriwa kukunja mil 10+ kila mmoja baada ya zoezi nzima kukamilika
Nyinyi sekta za kuwaajiri ni nyingi sana kijana tofauti na walimu. Sijui umeelewa?Mbona sisi kada nyingine tunafanya interview tatu ( written, practical, oral) na hatulii wala hatuundi chama....
Acheni kulia lia someni
Waseme ukweli nini hawataki na sio kuzunguka mbuyu …Kwaiyo unataka watu waendelee kufumbia macho tatizo liendelee kuwa kubwa kwa kigezo cha kuwa tatizo halijaanza leo bali limeanza zamani. Ndicho unachomaanisha mkuu?
Agenda zao hawa NETO zikizingatiwa kuna msululu wa NETO nyingine kwa Kada nyingine utakuja.Umoja wa Waalimu Wasio na Ajira (NETO) ulianza na Wanachama (wajumbe) 15 kupitia makundi ya WhatsApp. Tulianzisha NETO kwasababu ya sintofahamu ya ajira iliyopo kwa wahitimu kuanzia mwaka 2015 mpaka 2023.
Masuala ya usaili kumekuwa na changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikituumiza wasailiwa, changamoto hizi ni kubwa zimefika hatua zina athiri mpaka uchumi wetu moja kwa moja wasailiwa ambao ndio tuna maisha magumu mtaani, hawana ajira wanajitafuta kwa kiwango kidogo sana na kupata lakini wameathiriwa na huu usaili, wametumia gharama kubwa sana kiasi hatua ambayo wengine wameingia madeni.
Utafutaji wetu wa sisi ambao tumekosa ajira mtaani kwa kweli ni mgumu mno kiasi ambacho kupata 2,000/- kwa siku ya kula imekuwa ngumu. Baadhi ya watu wameenda kwenye usaili wakiwa wamechukua pesa kwa watu, mtu anaendesha pikipiki anaamua kukopa pesa ya kipande kwa bosi wake ili aweze kwenda kufanya usaijili Bahati mbaya hachaguliwi, hicho kitendo kina waumiza wengi. Lakini bado si hivyo tu kuna watu wanabiashara zao ndogo ndogo zimekufa kwasababu changamoto hii wanapoenda kufanya usaili ni mbali inatumika gharama kubwa kwahiyo imeathiri kwa kiwangu kikubwa hasa walala hoi ambao kwa asilimia kubwa hatuna biashara za msingi.
Katibu wa Umoja wa Waalimu Wasio na Ajira (NETO), Daniel Edgar, ameiomba Serikali kutoa ajira kwa wahitimu wa ualimu waliomaliza masomo yao kati ya mwaka 2015 na 2024.
Ameeleza kuwa kundi hilo lina kila sababu ya kuomba ajira, kwani wengi wao bado hawajapata nafasi ya kufanya kazi rasmi.
Aidha, Edgar ameitaka serikali kusimamia upangaji wa mishahara katika taasisi za elimu binafsi. Ameeleza kuwa kwa sasa, kuna tofauti kubwa katika malipo ya waalimu wa taaluma moja kulingana na ngazi tofauti za elimu, jambo ambalo linahitaji uangalizi wa serikali.
Amependekeza kuwa waalimu walipwe mishahara kulingana na kiwango chao cha elimu ili kuhakikisha haki inatendeka.
Wanawasilisha malalamiko yao ya Ajira
wanajulikana kama NETO
(None Employed Teacher Organisation)
Hao wakipewa mkeka watatawanyika woteWaache vijana wapambanie nafasi, chama Cha ma jobless kike wapa inspiration.
Mad Max, Mpaji Mungu mna kiona chama 🤣😂
Oya Anza kutembea na kisu, watekaji wame rudiHao wakipewa mkeka watatawanyika wote
Mimi ni mkulima niko zangu huku kibaoni nalima mahindi maisha yanasongaNyie ndio mkisha shibisha matumbo yenu hamuwajui wengine.
Na kudharau taaluma za watu, kwani hao madoctor wote wameajiriwa. Kwa mwendo wa ajira izi za CCM izamu yenu itafika tuu ni suala la muda.
Wa Kozi za Ualimu.Wahitimu wa nini
Wahaisibu, masekletari..??? Wewe tayari umeshafeli kabla ya interviewSiyo kweli kuna ofisi kibao hazina wahaisibu na makeshia wanatumia masekletari kufanya kazi hizo.
Kuna ofisi hazina ma IT ndiyo maana mafoleni kibao kazi haziendi.
Kuna maofisi hazina maprocurement manunuzi hovyo hovyo tuu.
Kuna zahanati hakuna Dr wanatibiwa na manesi.
Sema nyie mmezoea kupangiwa vituo hamjawahi ona intavyuu moyo kuruka ruka. Kuna watu toka 2012 mpaka sasa hawana kazi na wanafeli intavyuu lakini hawalalamiki.
Kada zingine mbona hawalalamiki? Waalimu huwa akili wanazipeleka wapi? Mnajidhalilisha sana.Mi nina mtazamo yofauti hapo:
Ilitakiwa serikali iwafikie kwa ukaribu hawa wanaosailiwa kuwapunguzia gharama.
Nina mtoto wa shangazi yangu amekaa morogoro almost 4 days akifanya hii kitu mnaitaa Usaili.
Gharama ni kubwa mtu job less hana kazi analipaje hizi gharama?
Amekusanya pesa kwenye biashara yake anakuja kuzika huku kwenye accomodation na malazi, Imagime boda boda wa watu kaacha kazi ya tajiri kaja huku.
Kuna walimu private wameathirika na kazia hii, boss akisikia umeomba ruhusa kwenda kufany interview anakula kichwa.
Kuna namna liangaliwe hili
Kwa hiyo, hiyo kazi unayosema ipo watapata au
DuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuhWanayo tayari ndo maana wana organization na wanachangishana, hao viongozi wana kipato toka kwa majobless!