DOKEZO Walimu Wasio na Ajira (NETO) wanaongea na waandishi wa habari kuondoa dukuduku lao

DOKEZO Walimu Wasio na Ajira (NETO) wanaongea na waandishi wa habari kuondoa dukuduku lao

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hawa vijana wakifanya mobilization vizuri na kwa akili serikali itawapigia magoti. Tatizo hiyo movement yao ni ya wachache huko wenzao wakiwa busy kubeti na kushangilia Simba na Yanga na usaliti wa Simba kwa Zuchu
Taratibu tu tutaelewana. Hata mbuyu ulianza kama mchicha.
 
Group tunazo nane saizi hadi zifike 30 huko, ikiwezekana na mabango tubebe tunawakaribisha ili msikie na hoja zingine
 
Wapuuzi hawa, wao wasifanyiwe usaili kwanini?
Kada zote kwa sasa, usaili ni lazima, many years ago, ndiyo usaili haukuwepo.
Wanajiona wao wanastahili sana kuliko wengine.
Sidhani kama wao huwa wanaulizwa kuanzia vya form one hadi chuo huko, afu wasome kwa week mbili au nne na kuvimaliza
 
Wapuuzi hawa, wao wasifanyiwe usaili kwanini?
Kada zote kwa sasa, usaili ni lazima, many years ago, ndiyo usaili haukuwepo.
Wanajiona wao wanastahili sana kuliko wengine.
Siyo wapuuzi. Punguza jazba, ushawahi ona wapi wasaili wa kada zingine unazozisema Wanasailiwa mkoa Kwa mkoa nchi nzima mwezi na siku kadhaa??
 
"Umoja wa Waalimu Wasio na Ajira (NETO) ulianza na Wanachama (wajumbe) 15 kupitia makundi ya WhatsApp. Tulianzisha NETO kwasababu ya sintofahamu ya ajira iliyopo kwa wahitimu kuanzia mwaka 2015 mpaka 2023."

"Masuala ya usaili kumekuwa na changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikituumiza wasailiwa, changamoto hizi ni kubwa zimefika hatua zina athiri mpaka uchumi wetu moja kwa moja wasailiwa ambao ndio tuna maisha magumu mtaani, hawana ajira wanajitafuta kwa kiwango kidogo sana na kupata lakini wameathiriwa na huu usaili, wametumia gharama kubwa sana kiasi hatua ambayo wengine wameingia madeni."

"Utafutaji wetu wa sisi ambao tumekosa ajira mtaani kwa kweli ni mgumu mno kiasi ambacho kupata 2,000/- kwa siku ya kula imekuwa ngumu. Baadhi ya watu wameenda kwenye usaili wakiwa wamechukua pesa kwa watu, mtu anaendesha pikipiki anaamua kukopa pesa ya kipande kwa bosi wake ili aweze kwenda kufanya usaijili Bahati mbaya hachaguliwi, hicho kitendo kina waumiza wengi. Lakini bado si hivyo tu kuna watu wanabiashara zao ndogo ndogo zimekufa kwasababu changamoto hii wanapoenda kufanya usaili ni mbali inatumika gharama kubwa kwahiyo imeathiri kwa kiwangu kikubwa hasa walala hoi ambao kwa asilimia kubwa hatuna biashara za msingi."

Katibu wa Umoja wa Waalimu Wasio na Ajira (NETO), Daniel Edgar, ameiomba Serikali kutoa ajira kwa wahitimu wa ualimu waliomaliza masomo yao kati ya mwaka 2015 na 2024.

Ameeleza kuwa kundi hilo lina kila sababu ya kuomba ajira, kwani wengi wao bado hawajapata nafasi ya kufanya kazi rasmi.

Aidha, Edgar ameitaka serikali kusimamia upangaji wa mishahara katika taasisi za elimu binafsi. Ameeleza kuwa kwa sasa, kuna tofauti kubwa katika malipo ya waalimu wa taaluma moja kulingana na ngazi tofauti za elimu, jambo ambalo linahitaji uangalizi wa serikali.

Amependekeza kuwa waalimu walipwe mishahara kulingana na kiwango chao cha elimu ili kuhakikisha haki inatendeka.

"Viongozi wetu wa Serikali, kutokana na uhalisia wa wahitimu na changamoto zinazoonekana katika zoezi la usaili kwa kada ya ualimu, tunapendekeza yafuatayo yafanyiwe kazi.

"Pendekezo la kwanza, kusitisha usaili mara moja kwa kada ya ualimu na kutumia utaratibu wa awali Pendekezo la pili, vyuo vimalize hatua zote za kumthibitisha mwalimu na siyo kuthibitishwa baada ya kukaa muda mrefu mtaani. Pendekezo la tatu, kusitisha uzalishaji wa walimu vyuoni hadi waliopo mtaani wapate Ajira"

Serikali inapata tabu sana kusimamia watanzania wenye akili kama za waalimu.
 
Mkuu mbona kwenye awamu ya 4 ya Jk waiting wa Ualimu walikua wanapata ajira moja kwa moja na wengi wao walikua hawataki kulipoti vituoni, Shida nini imepelekea ajira za walimu kua ngumu kuanzia awamu ya 5 mpaka sasa kwenye awamu hii?
Kada zote miaka mingi nyuma hakukuwa na usahili. Mtu upo shambani unaletewa barua ukaripoti kazini.
 
Siyo wapuuzi. Punguza jazba, ushawahi ona wapi wasaili wa kada zingine unazozisema Wanasailiwa mkoa Kwa mkoa nchi nzima mwezi na siku kadhaa??
Kupata kazi siyo lelemama kwa nyakati hizi hasa kwa mtoto wa mkulima,watu wamekwenda interviews za mbali zaidi ya mara 10,ndiyo wanatoboa, sembuse nyie tena mnazifanyia kila mtu mkoani kwake
 
Kupata kazi siyo lelemama kwa nyakati hizi hasa kwa mtoto wa mkulima,watu wamekwenda interviews za mbali zaidi ya mara 10,ndiyo wanatoboa, sembuse nyie tena mnazifanyia kila mtu mkoani kwake
Ndiyo tofauti ya walimu na ninyi/hao unaowasema. Mnakubalije kupelekwa pelekwa kizembe hivyo? Hii nchi ni yetu sote, basi kama unaona ni sahihi wawe wanarudishiwa gharama za Malazi, usafiri na accomodations zingine. Unakubaliaje kutiwa hasara kidenzi kiasi hicho?? Shutka hii nchi ni yetu sote.
 
Mkuu mbona kwenye awamu ya 4 ya Jk waiting wa Ualimu walikua wanapata ajira moja kwa moja na wengi wao walikua hawataki kulipoti vituoni, Shida nini imepelekea ajira za walimu kua ngumu kuanzia awamu ya 5 mpaka sasa kwenye awamu hii?
Wapo wengi we unataka waajiri tu bila uhitaji?
 
Ndiyo tofauti ya walimu na ninyi/hao unaowasema. Mnakubalije kupelekwa pelekwa kizembe hivyo? Hii nchi ni yetu sote, basi kama unaona ni sahihi wawe wanarudishiwa gharama za Malazi, usafiri na accomodations zingine. Unakubaliaje kutiwa hasara kidenzi kiasi hicho?? Shutka hii nchi ni yetu sote.
Mtu halazimishwi kwenda kwenye usaili,unapoenda ni kama mtafutaji, kuna kupata au kukosa.
So, kama mtu hataki usumbufu, ni bora asiende.
 
Mkuu mbona kwenye awamu ya 4 ya Jk waiting wa Ualimu walikua wanapata ajira moja kwa moja na wengi wao walikua hawataki kulipoti vituoni, Shida nini imepelekea ajira za walimu kua ngumu kuanzia awamu ya 5 mpaka sasa kwenye awamu hii?
Usiishi kwa mazoea,dunia inabadilika na ww badilika!!!
 
Hili kundi la walimu vilaza waliofeli usaili..asa hamtaki usaili mnataka kupitishwa kama makondooo...

Usaili ni muhimu sana kupunguza wapumbavu kwenye reli..tulieni mtazoea tuuu kama kada zengine.
 
Back
Top Bottom