DOKEZO Walimu Wasio na Ajira (NETO) wanaongea na waandishi wa habari kuondoa dukuduku lao

DOKEZO Walimu Wasio na Ajira (NETO) wanaongea na waandishi wa habari kuondoa dukuduku lao

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Yule mrombo ni very arrogant, ana egoism, anajiona anajua kila kitu, ameharibu elimu kuanzia mitaala. Ananyanyasa walimu anavyojisika ndio maana analalamikia protokali ya ikulu. Halafu kwanini watu wasiseme huu ni Rais wa kuambiwa.
Mama nae kaingia kwenye mfumo
 
Kwani serikali kutoa ajira kiduchu wameanza leo mbona kipindi hiki ndio maneno yamekua mengi
Kwaiyo unataka watu waendelee kufumbia macho tatizo liendelee kuwa kubwa kwa kigezo cha kuwa tatizo halijaanza leo bali limeanza zamani. Ndicho unachomaanisha mkuu?
 
Mi nina mtazamo yofauti hapo:
Ilitakiwa serikali iwafikie kwa ukaribu hawa wanaosailiwa kuwapunguzia gharama.

Nina mtoto wa shangazi yangu amekaa morogoro almost 4 days akifanya hii kitu mnaitaa Usaili.
Gharama ni kubwa mtu job less hana kazi analipaje hizi gharama?

Amekusanya pesa kwenye biashara yake anakuja kuzika huku kwenye accomodation na malazi, Imagime boda boda wa watu kaacha kazi ya tajiri kaja huku.

Kuna walimu private wameathirika na kazia hii, boss akisikia umeomba ruhusa kwenda kufany interview anakula kichwa.

Kuna namna liangaliwe hili
 

Umoja wa Waalimu Wasio na Ajira (NETO) ulianza na Wanachama (wajumbe) 15 kupitia makundi ya WhatsApp. Tulianzisha NETO kwasababu ya sintofahamu ya ajira iliyopo kwa wahitimu kuanzia mwaka 2015 mpaka 2023.

Masuala ya usaili kumekuwa na changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikituumiza wasailiwa, changamoto hizi ni kubwa zimefika hatua zina athiri mpaka uchumi wetu moja kwa moja wasailiwa ambao ndio tuna maisha magumu mtaani, hawana ajira wanajitafuta kwa kiwango kidogo sana na kupata lakini wameathiriwa na huu usaili, wametumia gharama kubwa sana kiasi hatua ambayo wengine wameingia madeni.

Utafutaji wetu wa sisi ambao tumekosa ajira mtaani kwa kweli ni mgumu mno kiasi ambacho kupata 2,000/- kwa siku ya kula imekuwa ngumu. Baadhi ya watu wameenda kwenye usaili wakiwa wamechukua pesa kwa watu, mtu anaendesha pikipiki anaamua kukopa pesa ya kipande kwa bosi wake ili aweze kwenda kufanya usaijili Bahati mbaya hachaguliwi, hicho kitendo kina waumiza wengi. Lakini bado si hivyo tu kuna watu wanabiashara zao ndogo ndogo zimekufa kwasababu changamoto hii wanapoenda kufanya usaili ni mbali inatumika gharama kubwa kwahiyo imeathiri kwa kiwangu kikubwa hasa walala hoi ambao kwa asilimia kubwa hatuna biashara za msingi.

Katibu wa Umoja wa Waalimu Wasio na Ajira (NETO), Daniel Edgar, ameiomba Serikali kutoa ajira kwa wahitimu wa ualimu waliomaliza masomo yao kati ya mwaka 2015 na 2024.

Ameeleza kuwa kundi hilo lina kila sababu ya kuomba ajira, kwani wengi wao bado hawajapata nafasi ya kufanya kazi rasmi.

Aidha, Edgar ameitaka serikali kusimamia upangaji wa mishahara katika taasisi za elimu binafsi. Ameeleza kuwa kwa sasa, kuna tofauti kubwa katika malipo ya waalimu wa taaluma moja kulingana na ngazi tofauti za elimu, jambo ambalo linahitaji uangalizi wa serikali.

Amependekeza kuwa waalimu walipwe mishahara kulingana na kiwango chao cha elimu ili kuhakikisha haki inatendeka.

Wanawasilisha malalamiko yao ya Ajira

wanajulikana kama NETO
(None Employed Teacher Organisation)

Agenda zao hawa NETO zikizingatiwa kuna msululu wa NETO nyingine kwa Kada nyingine utakuja.
 
Siyo kweli kuna ofisi kibao hazina wahaisibu na makeshia wanatumia masekletari kufanya kazi hizo.
Kuna ofisi hazina ma IT ndiyo maana mafoleni kibao kazi haziendi.
Kuna maofisi hazina maprocurement manunuzi hovyo hovyo tuu.
Kuna zahanati hakuna Dr wanatibiwa na manesi.
Sema nyie mmezoea kupangiwa vituo hamjawahi ona intavyuu moyo kuruka ruka. Kuna watu toka 2012 mpaka sasa hawana kazi na wanafeli intavyuu lakini hawalalamiki.
Wahaisibu, masekletari..??? Wewe tayari umeshafeli kabla ya interview
 
Mi nina mtazamo yofauti hapo:
Ilitakiwa serikali iwafikie kwa ukaribu hawa wanaosailiwa kuwapunguzia gharama.

Nina mtoto wa shangazi yangu amekaa morogoro almost 4 days akifanya hii kitu mnaitaa Usaili.
Gharama ni kubwa mtu job less hana kazi analipaje hizi gharama?

Amekusanya pesa kwenye biashara yake anakuja kuzika huku kwenye accomodation na malazi, Imagime boda boda wa watu kaacha kazi ya tajiri kaja huku.

Kuna walimu private wameathirika na kazia hii, boss akisikia umeomba ruhusa kwenda kufany interview anakula kichwa.

Kuna namna liangaliwe hili
Kada zingine mbona hawalalamiki? Waalimu huwa akili wanazipeleka wapi? Mnajidhalilisha sana.
 
Hao viongozi watapewa Tshirt chap, watasaliti wenzao chap!
 
Back
Top Bottom