DOKEZO Walimu watakiwa kuhudhuria mafunzo ya mtaala mpya kwa siku 2 kwa malipo ya Tsh. 3,000 kwa siku!

DOKEZO Walimu watakiwa kuhudhuria mafunzo ya mtaala mpya kwa siku 2 kwa malipo ya Tsh. 3,000 kwa siku!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kuna siku msonde aliwahi itisha kikao tena jumapili watu wanatoka umbali mrefu hata nauli wala chai hawakupata.
Sioni ajabu wala
 
Huu ni uzushi, wakurugenzi hawezi kuwadhalilisha walimu namna hii. Elfu sio kiwango cha fedha kwa chakula cha watumishi wa ngzi yoyote ile. Serikali ikanushe uchonganishi huu haraka.
Rejea post yangu hapo juu,kipi kimekushangaza?
 
Serikali imebadili mtaala na kuanzia mwaka huu, wanafunzi wa kidato cha kwanza wataanza kusoma mtaala mpya. Hivyo Serikali imeamua kuwapa semina walimu ili kuendana na kasi ya mtaala mpya.

Walimu kutoka Halmashauri X wametakiwa kuhudhuria semina ya mtaala mpya ambapo malipo yao ni sh. Elfu tatu kwa siku.

Mafunzo hayo yatakayofanyika kwa siku mbili jumla kila mwalimu atalipwa kitita cha sh. 6,000/=

Mimi ni mjumbe tu, na mjumbe hauwawi.

Kwani hadi mpewe posho ndio mhudhurie mafunzo? Tabia mbaya ya kizembe! Wewe ndiye unapata mafunzo halafu unataka na posho! Anayetoa mafunzo ndiye anapaswa apate posho.
 
Kwani hao wenzetu wanatumia mwongozo gani wa kulipa Posho?

Kwa mujibu wa mwongozo wa Wizara ya Fedha/Hazina

Posho huwa ni shilingi 80,000-250,000 Kwa Siku

Hiyo ya elfu 3, ndiyo naona Mwaka huu 🙌

Kweli Walimu hawapendani 🙌
Kwamba kuna anaezifyeka?
 
Huu ni uzushi, wakurugenzi hawezi kuwadhalilisha walimu namna hii. Elfu sio kiwango cha fedha kwa chakula cha watumishi wa ngzi yoyote ile. Serikali ikanushe uchonganishi huu haraka.
Watu wafupi huwa mnakuwaga wabishi!! Jina lako linasadifu
 
Mtaala ushaanza kufeli ,tumehudhuria
Semina majuzi,hawakutupa taarifa kama hii mwanzoni nilienda kwenye semina januari hii jinsi inavyokuwa ngumu kwa kutumia nauli yangu ,imeishia kupotea na sikupewa chochote,.na jambo moja ninaloliona ualimu unadharauliwa na Kila mtu.
 
Kweli mfano ustawi chini ya manispaa kikao cha ndani cha kawaida 40000 per day iko kinasimamiwa na manispaa nje ya manispa mfano now wiki ya sheria kutoa elimu per day 50000 na upo ndani ya manispaa ukitoka na hapo bado mashirika yalio zamini hawaja wasainisha unakuta shirika moja linawasainisha 100000 per day sijawai ona mtu wa ustawi kasain posho ya 20000 kushuka chini
Halmashauri gani hiyo?..mbona Mimi nimeenda tukapigwa 50000 per day? Na ni siku 3?
 
kama wanapata molo wa kutwa na vituo viko karibu na maeneo yao ya kazi sioni tatizo apo
 
Back
Top Bottom