DOKEZO Walimu watakiwa kuhudhuria mafunzo ya mtaala mpya kwa siku 2 kwa malipo ya Tsh. 3,000 kwa siku!

DOKEZO Walimu watakiwa kuhudhuria mafunzo ya mtaala mpya kwa siku 2 kwa malipo ya Tsh. 3,000 kwa siku!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Bora hiyo elfu tatu. Mwaka jana walipewa maji ya kikao basi..

Ila walimu sijui nani aliwaloga kwakweli.

Na hapo sasa utakuta wamejazana haswa .

Hushangaii walimu wana miezi sita hawajalipwa shule flani hata mia ila wapo tuuu.. Daah
Ni viumbe wa aina yao na wao...
 
Sana na sijui kwanini hawawazingatii
Labda Uelewa wao mdogo ama mfumo walionao unawabana zaidi

Ila ingekuwa Wana umoja, lazima wangebadirishiwa maslahi yao

Changamoto waliyonayo, Kila Mtumishi amekuwa boss wa Mwalimu

Yaani Afisa mtendaji, Afisa Elimu Kata, Afisa kutoka Halmashauri, DEOs, Mkurugenzi wa Halmashauri, Diwani, Mwenyekiti wa Kijiji n.k 🙌
 
Ni sawa na kulipwa chips kavu, mshikaki mmoja na mirinda nyeusi ya bariiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiidi
Chips kavu kwa sasa ni buku mbili na soda ni 700 na mshikaki ni buku hivyo 3000 haitoshi 😂😂😂😂😂😂
 
Serikali imebadili mtaala na kuanzia mwaka huu, wanafunzi wa kidato cha kwanza wataanza kusoma mtaala mpya. Hivyo Serikali imeamua kuwapa semina walimu ili kuendana na kasi ya mtaala mpya.

Walimu kutoka Halmashauri X wametakiwa kuhudhuria semina ya mtaala mpya ambapo malipo yao ni sh. Elfu tatu kwa siku.

Mafunzo hayo yatakayofanyika kwa siku mbili jumla kila mwalimu atalipwa kitita cha sh. 6,000/=

Mimi ni mjumbe tu, na mjumbe hauwawi.

Duh elfu sita
 
Mbona nyingi sana?

Kikubwa wasisahau kuvaa sale za kijani.
Na kazi inendeleee
 
Hii kazi mama angu mzazi hakuwa anaifurahia kabisa ..kwa maisha tuliy9kuwa tunaishi alitushauri kabisa asitokee mmoja wetu akasomea hii kazi tena...aliomba kutaafu mapema kabla muda akafanya mishe zake nyingine ...
 
Labda Uelewa wao mdogo ama mfumo walionao unawabana zaidi

Ila ingekuwa Wana umoja, lazima wangebadirishiwa maslahi yao

Changamoto waliyonayo, Kila Mtumishi amekuwa boss wa Mwalimu

Yaani Afisa mtendaji, Afisa Elimu Kata, Afisa kutoka Halmashauri, DEOs, Mkurugenzi wa Halmashauri, Diwani, Mwenyekiti wa Kijiji n.k 🙌
Basi ndio maana wanawamudu na kuwapelekesha watakavyo.
 
Jamaa yangu Arusha kasema mafunzo yatafanyika Jan 30-31 kwa walimu wote wa public na private wanaofundisha form one, na posho ndio hiyo. Ni huzuni na fezea
 
Back
Top Bottom