Walinzi Arusha wafunga mageti na kuondoka kwenye hospitali kubwa Seliani, wanadai milioni 42

Kuna siku nlisika waliiweka bond wakachukua B9 afu waumini wakaja kulipa
 
KKKT shida nini mpaka mnakosa hela za kulipa..?
Katibu mkuu wa hio diocese anafanya kazi gani sasa ofisini.??
Ana fanya kazi ya kuji lipa pesa ndefu ..hili kanisa ni kama chama cha siasa .ni vurugu ndani kwa ndani
 
Pesa kwaajili ya walinzi kila siku ni karibia 234,000 Kwa wiki 1,638,000 Swali fikirishi kwanini wanawalinzi wengi
 
Changamoto ya hospitali za dini haipo kkkt peke yake,hospitali nyingi za misheni zinachechemea, kuongezeka kwa vituo vingi vya afyabcya serikali kumepelekea kupungua kwa wateja, bima ya afya na ongezeko la polyclinics
 
Changamoto ya hospitali za dini haipo kkkt peke yake,hospitali nyingi za misheni zinachechemea, kuongezeka kwa vituo vingi vya afyabcya serikali kumepelekea kupungua kwa wateja, bima ya afya na ongezeko la polyclinics
Serikali inawapelekea moto kimyakimya. Mwisho wao umefika baada ya kuwapiga sana wananchi huku wakijifanya wanasaidia. Mimi ninashauri hospitali ya Seliani igeuzwe kuwa Hotel kwasababu huduma zao ni za hovyo.
 
Ana fanya kazi ya kuji lipa pesa ndefu ..hili kanisa ni kama chama cha siasa .ni vurugu ndani kwa ndani
Kujilipa pesa kubwa sio shida ila managing ya hospital inabidi iwe vizuri.
 
Ndo maana wakatoliki Papa wao alisoma upepo akakataza mapadri kuoa,,,,,,kua na familia na huna sehem yeyote ya kuingiza kipato zaidi ya kutegemea kanisa inakua msala,,,,,,Jamaa matumizi yamekua makubwa kuliko kinachoingia, na kinachoingia kinamendewa na wengi,Padri anataka goodlife na familia yake afanyaje sasa
 
Hospital nyingi zinategemea mapato ya bima hasa bima ya NHIF. Kwa sasa bima wamekuwa hawalipi kwa wakati hivyo kupelekea hospitali kuchechemea. Ikumbukwe BIMA inasimama kama mtu kati kati ya mgonjwa na hospitali. Hivyo mtu anapopata huduma inatakiwa BIMA ilipe kwa wakati. Sasa unapochukua miezi mpaka sita pasipo malipo wakati mgonjwa kashapata huduma unategemea utaendesha vipi hospitali?

kwa sasa vituo vingi vya afya visivyo kuwa na ruzuku ya Serikali vina hali mbaya sana
 
Hiyo hospitali ilishaanza kuzorota kutoa huduma nzuri toka kitambo.Kuna kipindi watu walikua wanahiita selian hotel,kwamba huduma za chakula kwa mgonjwa aliyelazwa zilikua nzuri kuliko huduma za matibabu.Kwahiyo hiyo yakutolipa wafanyakazi inawezekana ni matokeo ya kuzorota kwa huduma kulikoanza miaka kadhaa nyuma ila kukafumbiwa macho.
 
Hili la bima nadhan waziri na viongozi husika wa huo mfuko uwezo wao umeshaisha imebaki porojo za kisiasa na kulindana.maana kila mara malalamiko ni yale yale.
 
Unakuta kiongozi wa dini sadaka anabeba,

Pesa za hospital kwenye vikao Nako pia anahitaji posho Nene hapo kitabaki nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…