KERO Walinzi mgodi wa Magesa hatujalipwa mishahara zaidi ya miezi 3, muhusika anasema hawezi lipa sababu kazi zilisimama, lakini kazi za ulinzi hazikukoma

KERO Walinzi mgodi wa Magesa hatujalipwa mishahara zaidi ya miezi 3, muhusika anasema hawezi lipa sababu kazi zilisimama, lakini kazi za ulinzi hazikukoma

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nina fanya kazi kazi katika Mgodi wa Magesa Gold mine uliopo Nyamatagata wilaya ya Geita mkoani Geita.

Changamoto iliyopo ni kwamba; tuna zaidi ya miezi mitatu (3) hatujapata mishahara, mgodi ulikuwa umesimama uzalishaji kutokana na changamoto ya mvua zilizokuwa zinaendelea kunyesha lakini sisi tuliendelea na kazi kwa sababu sisi tupo kwenye sekta ya ulinzi.

Mhusika anadai hawezi kulipa pesa kwa sasa kwa sababu kazi hazifanyiki na sisi hatuna pesa yeyote ile na hataki hata kuongea na sisi.

Tunaomba mamlaka husika au serikali watusaidie.
 
Tunaomba msaada zaidi wafanyakazi kazi Mgodi wa Magesa Gold mine uliopo Nyamatagata wilaya ya Geita mkoani GEITA changamoto iliyopo tuna zaidi ya miezi mitatu 3 hatujapata mishahara yetu Mhusika wa mgodi ambaye ni mkurugenzi, hataki kulipa
 
Nimeona nyuzi kibao kuhusu malalamiko ya walinzi juu ya mishahala yao inaonekana hili ni tatizo sugu, na wanachukuliwa poa sana.
 
Back
Top Bottom