Walinzi wa Freeman Mbowe walikuwa wapi wakati akishambuliwa na ni kweli alipokewa hospitalini akiwa amelewa chakari?

Richard

Platinum Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
16,890
Reaction score
26,440
Kwanza nitoe pole kwa mheshimiwa Freeman Mbowe kwa kushambuliwa na watu wasojulikana na kisha kuumizwa mguu.

Namtakia ahueni na apone haraka kisha kurudi bungeni kuendelea na shughuli za upinzani.

Taarifa zinazozagaa kwa kasi mjini Dodoma ni kwamba mheshimiwa Mbowe hakuwa na walinzi alipokuwa akirudi kutoka kwenye shughuli zake binafsi.

Pia taarifa hizo zinaendelea kudai kwamba mheshimiwa Mbowe alipokelewa hospitalini akiwa amelewa pombe chakari.

Kama polisi watathibitisha habari hizi khasa hii ya kulewa pombe, basi habari za kushambuliwa kwa Mbowe ambazo zilitumwa kwa kasi ya umeme kwa baadhi ya sehemu muhimu kwa upinzani ukiwemo umoja wa Ulaya na Ubalozi wa Uingereza zitakuwa zimeingia dosari.

Je, vipi juu ya taratibu za ulnzi kwa viongozi wakuu wa upinzani mbone zimekuwa hazitiliwi maanani khasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu?

Pia kuna taarifa kwamba watu wasojulikana ambao wamemshambulia mheshimiwa Mbowe walisikika wakisema kwamba mbona anaisumbua serikali ?

Taarifa hizi zimetolewa hadi bungeni huku wabunge kadhaa akiwemo mheshimiwa Lusinde akitoa madai ya mheshimiwa Mbowe kupokelewa na madaktari akiwa amelewa chakari.

Ikiwa watu wasojulikana wana ushahidi wote juu ya matendo ambayo mheshimiwa Mbowe anayaratibu mbona hawatoi taarifa polisi ambao watachunguza na kisha kuwafikisha mahakamani wahusika wote.

Lakini masuali ya msingi ni kwamba kwanini mheshimiwa Mbowe hakuwa na ulinzi alipokuwa kwenye mizunguko yake.

Je, ni kweli mheshimiwa Mbowe alipokuwa hospitalini akiwa amelewa chakari?
 
Hata chadema hawajatoa taarifa rasmi,hawana cha kuwaongopea wananchi
Hili suala la kuchepuka wanaume si ajabu,lakini kutafuna wake za watu,ona sasa Mungu alivyofundi,kaanguka akiwa na mke wa mtu,hata wakisema kashambuliwa,bado mke wa mtu alikuwepo itabidi aeleze ilikuaje,haiwezekani kumkimbiza mke wa mtu ughaibuni,ndio maana kina mnyika wamenywea
 
Taarifa zinazagaa kwa kasi hapo Dodoma kivipi wakati ni taarifa ambazo zimetolewa na Ndugai ndani ya Bunge akiwatumia baadhi ya wabunge wake maalumu?

Kulewa mtu ama kutolewa is not an issue of debate here. Kila mtu ana haki ya kuishi na kutotendewa vibaya kinyume cha sheria bila kujali mtu huyo ni mlevi, kahaba ama vyovyote vile so long as hakuna sheria iliyovunjwa kwa mtu kutumia uhuru wake binafsi....

Kikubwa hapa ni kuwa mtu kashambuliwa na kuumizwa. Kama ni kunywa pombe, Mbowe ni wazi hakuanza jana kunywa hizo pombe. Kama ndivyo kwanini iwe ishu na iwe kisingizio cha watu kutowajibika kwa matendo yao?

Tunachotaka polisi wachunguze na waje na ripoti credible isiyo na story za kisiasa za kupewa na kina Ndugai.....

By the way, majeraha ya mtu aliyeanguka kwa bahati mbaya popote kwa sababu zozote zile yana tofauti kubwa na ya kushambuliwa kwa lengo la kudhuru....

After all, kila mtu anajua jinsi serikali isivyompenda Freeman Mbowe na chama chake - CHADEMA...

Ushahidi upo wa Rais wa nchi huyuhuyu John Pombe Magufuli akiapa kufuta vyama tishio kwake mwaka huu 2020 CHADEMA ikiwemo...

Sasa ni uwazi ulio shahiri dhahiri kuwa kashindwa kutimiza azma yake hiyo....

Kashindwa kwa kutumia hoja za kisiasa majukwaani kuwashawishi watu waifute CHADEMA mioyoni mwao japokuwa kwa miaka mitano yote ni yeye tu na CCM yake ndo walikuwa kiguu na njia wakifanya siasa....;

Kashindwa kwa kutumia njia za kisheria na kimahakama.....

Kashindwa kwa kutumia mbinu zote za kisiasa za halali na haramu. Sasa ameamua kutumia nguvu ya Risasi na ujambazi wa waziwazi mchana kweupe kwa kudhani watu ni wajinga....

Sasa anamtumia Spika Ndugai. Lakini yeye ndiye hopeless kabisa maana anajionesha waziwazi kuwa yupo kwenye misheni maalumu ya mapambano kwa kutumia madaraka yake ya u - Spika...

Leo bila aibu na kama anawaelekeza polisi nini cha kufanya cha kusema baadae kwenye ripoti yao, anabwatuka ndani ya bunge kutoa taarifa za kitabibu na hitimisho juu jambo hili kana kwamba yeye ni mchunguzi polisi...

Kwa hakika, hii "desperation" walio nayo wenye jukumu hili, ni ishara kuwa wako tayari kunywa damu ya mtu wanayemchukua mchana kweupe hawa....!!
 
Kumbe ni Ahmada?
Ahmada amelewa
IMG-20200609-WA0015.jpg
 
Kwanza nitoe pole kwa mheshimiwa Freeman Mbowe kwa kushambuliwa na watu wasojulikana na kisha kuumizwa mguu.

Namtakia ahueni na apone haraka kisha kurudhi bungeni kuendelea na shughuli za upinzani.

Taarifa zinazozagaa kwa kasi mjini Dodoma ni kwamba mheshimiwa Mbowe hakuwa na walinzi alipokuwa akirudi kutoka kwenye shughuli zake binafsi.

Pia taarifa hizo zinaendelea kudai kwamba mheshimiwa Mbowe alipokelewa hospitalini akiwa amelewa pombe chakari.

Kama polisi watathibitisha habari hizi khasa hii ya kulewa pombe, basi habari za kushambuliwa kwa Mbowe ambazo zilitumwa kwa kasi ya umeme kwa baadhi ya sehemu muhimu kwa upinzani ukiwemo umoja wa Ulaya na Ubalozi wa Uingereza zitakuwa zimeingia dosari.

Je, vipi juu ya taratibu za ulnzi kwa viongozi wakuu wa upinzani mbone zimekuwa hazitiliwi maanani khasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu?

Pia kuna taarifa kwamba watu wasojulikana ambao wamemshambulia mheshimiwa Mbowe walisikika wakisema kwamba mbona anaisumbua serikali ?

Taarifa hizi zimetolewa hadi bungeni huku wabunge kadhaa akiwemo mheshimiwa Lusinde akitoa madai ya mheshimiwa Mbowe kupokelewa na madaktari akiwa amelewa chakari.

Ikiwa watu wasojulikana wana ushahidi wote juu ya matendo ambayo mheshimiwa Mbowe anayaratibu mbona hawatoi taarifa polisi ambao watachunguza na kisha kuwafikisha mahakamani wahusika wote.

Lakini masuali ya msingi ni kwamba kwanini mheshimiwa Mbowe hakuwa na ulinzi alipokuwa kwenye mizunguko yake.

Je, ni kweli mheshimiwa Mbowe alipokuwa hospitalini akiwa amelewa chakari?
Kwanini nawakala wa ccm humu wana matope kichwani ?
 
Taarifa zinazagaa kwa kasi hapo Dodoma kivipi wakati ni taarifa ambazo zimetolewa na Ndugai ndani ya Bunge akiwatumia baadhi ya wabunge wake maalumu?

Kulewa mtu ama kutolewa is not an issue of debate here. Kila mtu ana haki ya kuishi na kutotendewa vibaya kinyume cha sheria bila kujali mtu huyo ni mlevi, kahaba ama vyovyote vile....

Kikubwa hapa ni kuwa mtu kashambuliwa na kuumizwa. Kama ni kunywa pombe, Mbowe ni wazi hakuanza jana kunywa hizo pombe. Kama ndivyo kwanini iwe ishu na iwe kisingizio cha watu kutiwajibika kwa matendo yao?

Majeraha ya mtu aliyeanguka kwa bahati mbaya popote kwa sababu zozote zile hana tofauti kubwa na ya kushanbuliwa kwa lengo la kudhuru....

After kila mtu anajua jinsi serikali isivyompenda Freeman Mbowe na chama chake - CHADEMA na ushahidi upo wa Rais wa nchi huyuhuyu John Pombe Magufuli akiapa kuifuta....

Kashindwa kwa kutumia hoja za majukwaani; kashindwa kwa kutumia njia za kisheria na kimahakama. Kashindwa kwa kutumia mbinu zote za kisiasa. Sasa ameamua kutumia nguvu ya Risasi na Ujambazi....

Sasa anamtumia Spika Ndugai. Lakini yeye ndiye hopeless kabisa maana anajionesha waziwazi kuwa yupo kwenye misheni maalumu ya mapambano kwa kutumia madaraka yake ya u - Spika...

Leo bila aibu na kama anawaelekeza polisi nini cha kufanya na kusema baadae kwenye ripoti yao, anabwatuka ndani ya bunge kutoa taarifa za kitabibu na hitimisho juu...

Kwa hakika, hii "desperation" walio nayo wenye jukumu hili, ni ishara kuwa wako tayari kunywa damu ya mtu nchana kweupe hawa....!!

Mbowe ni "public figure", kwanini hakuwa na walinzi wake wakti alipokumbwa na masahibu ya kipigo?
 
Taarifa zinazagaa kwa kasi hapo Dodoma kivipi wakati ni taarifa ambazo zimetolewa na Ndugai ndani ya Bunge akiwatumia baadhi ya wabunge wake maalumu?

Kulewa mtu ama kutolewa is not an issue of debate here. Kila mtu ana haki ya kuishi na kutotendewa vibaya kinyume cha sheria bila kujali mtu huyo ni mlevi, kahaba ama vyovyote vile so long as hakuna sheria iliyovunjwa kwa mtu kutumia uhuru wake binafsi....

Kikubwa hapa ni kuwa mtu kashambuliwa na kuumizwa. Kama ni kunywa pombe, Mbowe ni wazi hakuanza jana kunywa hizo pombe. Kama ndivyo kwanini iwe ishu na iwe kisingizio cha watu kutowajibika kwa matendo yao?

Tunachotaka polisi wachunguze na waje na ripoti credible isiyo na story za kisiasa za kupewa na kina Ndugai.....

By the way, majeraha ya mtu aliyeanguka kwa bahati mbaya popote kwa sababu zozote zile yana tofauti kubwa na ya kushambuliwa kwa lengo la kudhuru....

After all, kila mtu anajua jinsi serikali isivyompenda Freeman Mbowe na chama chake - CHADEMA...

Ushahidi upo wa Rais wa nchi huyuhuyu John Pombe Magufuli akiapa kufuta vyama tishio kwake mwaka huu 2020 CHADEMA ikiwemo...

Sasa ni uwazi ulio shahiri dhahiri kuwa kashindwa kutimiza azma yake hiyo....

Kashindwa kwa kutumia hoja za kisiasa majukwaani kuwashawishi watu waifute CHADEMA mioyoni mwao japokuwa kwa miaka mitano yote ni yeye tu na CCM yake ndo walikuwa kiguu na njia wakifanya siasa....;

Kashindwa kwa kutumia njia za kisheria na kimahakama.....

Kashindwa kwa kutumia mbinu zote za kisiasa za halali na haramu. Sasa ameamua kutumia nguvu ya Risasi na ujambazi wa waziwazi mchana kweupe kwa kudhani watu ni wajinga....

Sasa anamtumia Spika Ndugai. Lakini yeye ndiye hopeless kabisa maana anajionesha waziwazi kuwa yupo kwenye misheni maalumu ya mapambano kwa kutumia madaraka yake ya u - Spika...

Leo bila aibu na kama anawaelekeza polisi nini cha kufanya cha kusema baadae kwenye ripoti yao, anabwatuka ndani ya bunge kutoa taarifa za kitabibu na hitimisho juu jambo hili kana kwamba yeye ni mchunguzi polisi...

Kwa hakika, hii "desperation" walio nayo wenye jukumu hili, ni ishara kuwa wako tayari kunywa damu ya mtu wanayemchukua mchana kweupe hawa....!!

Unatia kinyaaa. Karudie kusoma hata UPE. Umeandika gazeti refu na kutuhumu kipumbavu. Ndo mana watu wa aina yako hawataweza kuaminika. Hambadiliki na mazingira. I pity you.
 
Ushaambiwa alikuwa na goma yuko bwii anaenda kuruka ndebe hao walinzi wamletee gozi.

Ina maana CHADEMA hawazingatii masuala ya personal protection?

Huwa ianatakiwa kuacha nafasi kidogo kati ya mlindwa na walinzi.
 
Apa ndo nachukiaga siasa, kutia watu vilema sio mpango kabisa.
 
Inavyoelekea Mheshimiwa Spika alienda kumpa pole lakini kutokana na hali aliyomkuta nayo akatilia shaka kuumia kwake. Inaelekea alipokuwa anaongea nae alihisi kuwa amelewa au alilewa. Hiyo ikamfanya atume madaktari wake wakafanye uchunguzi zaidi. Madaktari hao wakampa taarifa kuwa KUB alipofika alikuwa amelewa chakari na kuwa hakuumia sana. Ninachojiuliza ni kuwa hali ya mgonjwa si inatakiwa kuwa siri yake na daktari wake? Aidha, walitumia vipimo gani kuwa hali ile ya kulewa ilitokana na pombe na sio dawa aliyopewa alipofika hospitali?

Amandla...
 
Back
Top Bottom