Mbowe ni "public figure", kwanini hakuwa na walinzi wake wakti alipokumbwa na masahibu ya kipigo?
Kwani wewe hapo ulipo siyo public figure? Una walinzi wa kukulinda?
Je, kwa kuwa huna walinzi ni halali utendewe unyama, ushambuliwe?.... Hili swali lako liko out of context. Halima maana kwa sasa....
Na kwani mtu akitendewa uhalifu ni nini kinapaswa kufanyika kwa mujibu wa sheria?
Ndugu, jambo la muhimu na la msingi kwa sasa ni hili:
Mtu kadai kavamiwa na kupigwa na kuumizwa. Anasema kafanyiwa uhalifu na wahalifu hao walikuwa na lengo la kumdhuru ama kumuua kabisa....
Kumshambulia mtu mwingine kwa nia kudhuru mwili ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria zetu....
Kimsingi uhalifu unadhibitiwa na jeshi la polisi kwa mujibu wa kisheria....
Linapotokea tukio kama hili, hatua ya kwanza ni uchunguzi wa polisi....
Uchunguzi ni " process" inayopitia na kuangalia mambo mengi ikiwemo hata hiki unachouliza....
Mwisho through uchunguzi, wahalifu (perpetrators) wanaweza kukamatwa na kuwa held accountable kwa mujibu wa sheria...
Likifanyika hili, hata swali lako hili (Japo mi binafsi naliona siyo la muhimu) jibu lake litakuwa addressed na matokeo ya uchunguzi huo...
Cha muhimu ktk stage hii ni uchunguzi wa kipolisi kujikita kujibu swali la:
Je, hili ni tukio la kihalifu ama ni ajali ya kawaida?